• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:50 AM
Lampard arithi tena masaibu aliyoacha Chelsea

Lampard arithi tena masaibu aliyoacha Chelsea

Na MASHIRIKA

FRANK Lampard alianza vibaya awamu yake ya pili ya ukufunzi kambini mwa Chelsea kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Wolverhampton Wanderers kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugani Molineux, Jumamosi.

Bao la pekee katika pambano hilo lilijazwa kimiani na Matheus Nunes aliyecheka na nyavu kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe na Wolves kutoka Sporting Lisbon ya Ureno kwa Sh6.2 bilioni mnamo Agosti 2022.

Ilikuwa mechi ya tatu mfululizo kwa Chelsea kukamilisha bila kufunga bao na mchuano wao wa 11 kupoteza katika EPL muhula huu. Miamba hao waliotawazwa wafalme wa EPL mnamo 2016-17 sasa hawajafunga bao katika mechi 12 ligini msimu huu na wanakamata nafasi ya 11 jedwalini kwa alama 39 baada ya kushinda mechi mbili pekee kati ya 11 zilizopita.

Hatua ya Lampard kuwajibisha Raheem Sterling na Conor Gallagher katika safu ya mbele ilikosa kuzaa matunda na badala yake wanasoka hao wawili wakaonyeshwa kadi za manjano.

Pierre-Emerick Aubameyang naye alipangwa katika kikosi cha akiba na mvamizi huyo raia wa Gabon akapata tumaini la kuchezea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu Februari 26.

Lampard sasa ana mtihani mgumu wa kunyanyua Chelsea watakaoelekea Uhispania mnamo Aprili 12, 2023 kuvaana na Real Madrid katika mkondo wa kwanza wa robo-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Son Heung-min mwanasoka wa kwanza kutoka Asia kufunga mabao...

Wanafunzi wawili wakamatwa wakishukiwa kuteketeza bweni

T L