• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Leads United inapigiwa chapuo kufanya kweli

Leads United inapigiwa chapuo kufanya kweli

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Leads United inapigiwa chapuo kuzamisha Ngamia One FC na kusonga mbele kwenye mechi za kuwania taji la Tim Wanyonyi Super Cup 2021 katika uga wa UoN CAVS, Nairobi.

Nao wachana nyavu wa Kibagare Slums wamepangwa kuchuana na Wazoefu FC huku Potters ikigarazana na Buffalo FC uwanjani humo. Wazoefu FC itashiriki mchezo baada ya kuangusha Lopez FC kwa mabao 5-0. Leads United ya kocha, Wilston Issa inapigiwa upatu kuendeleza ubabe wake kwenye kampeni hizo baada ya kunyamazisha Kibagare Sportiff kwa bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza.

”Katika mpango mzima tunataka tujikaze kiume tuhakikishe tunashinda mechi zote na kutwaa tiketi ya fainali ya mwaka huu ambapo tumepania kuhifadhi kombe hilo,” kocha huyo wa Leads alisema. Leads United ambayo hushiriki Ligi ya Taifa Daraja la Pili inajivunia huduma za sajili wapya wanaotazamiwa kuchochea wenzao kwenye michezo hiyo.

Timu inategemea wachana shupavu kama Kelvin Juma, Herman Ngala, Benito Kambele, Bernard Odhiambo, Michael Onyango na Calvin Odhiambo kati ya wengine.

Kwenye ratiba ya mechi hizo katika uga wa Kihumbu-ini, Kangemi Nairobi, Kangemi Atletico imepangwa kumenyana na CAVS nayo Simba FC itaumana na Kabete Technical FC huku wachezaji wa Dreams FC wakipepetana na Kitusuru Allstars.

ISSA: Kocha wa Leads United, Wilston Issa akiongea na wachezaji baada ya kushinda mchezo mmoja kwenye kampeni za kuwania taji la Tim Wanyonyi Super Cup…
Picha/JOHN KIMWERE

Kangemi Atletico ilinasa tiketi ya kushiriki patashika hiyo iliposajili ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Gachie Youth. Mashindano ya mwaka huu ambayo ni makala ya nane yalivutia jumla ya timu 64 za wanaume na 14 za wanawake. Leads United na Kibagare Girls ndio mabingwa watetezi kitengo cha wanaume na wanawake mtawalia.

Leads ilibeba taji hilo ilipogaragaza Leverkusen FC mabao 4-2 kupitia mipigo ya matuta baada ya kutoka bao 1-1.


Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

Rais Kenyatta ahutubia taifa kupitia kikao cha pamoja...

SHINA LA UHAI: Saratani ya mifupa inayolemaza waathiriwa

T L