• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
Leicester wapata beki wa kuziba pengo la Fofana aliyevunjika mguu

Leicester wapata beki wa kuziba pengo la Fofana aliyevunjika mguu

Na MASHIRIKA

LEICESTER City wamemsajili beki raia wa Denmark, Jannik Vestergaard kutoka Southampton.

Vestergaard, 29, alichezea Southampton mara 79 baada ya kujiunga na kikosi hicho kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani mnamo 2018. Anaingia katika sajili rasmi ya Leicester ambao ni washikilizi wa Kombe la FA kwa mkataba wa miaka mitatu.

Anakuwa beki wa pili kusajiliwa na Leicester kutoka Southampton muhula huu baada ya Ryan Bertrand aliyeingia ugani King Power mnamo Julai 2021.

Uhamisho huo wa Vestergaard unamuunganisha na Kasper Schmeichel ambaye ni kipa chaguo la kwanza la Denmark.

Vestergaard ambaye amechezea Denmark mara 29, aliwajibishwa katika michuano sita iliyosakatwa na Denmark hadi kufikia nusu-fainali ya Euro 2020 mnamo Juni-Julai 2021.

Kusajiliwa kwake kulichochewa na haja ya Leicester kujaza pengo la beki Wesley Fofana atakayesalia nje kwa muda mrefu baada ya kuvunjika mguu mwanzoni mwa wiki hii dhidi ya Villarreal kirafiki.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

UMBEA: Uvumilivu una kikomo chake, chunga usije ukala...

Wakazi wahofia vita vya jamii za wafugaji