• Nairobi
  • Last Updated June 1st, 2023 12:23 AM
Lionel Messi abeba PSG dhidi ya Toulouse katika Ligi Kuu ya Ufaransa

Lionel Messi abeba PSG dhidi ya Toulouse katika Ligi Kuu ya Ufaransa

Na MASHIRIKA

BAO la kiufundi kutoka kwa Lionel Messi lilisaidia Paris Saint-Germain (PSG) kutoka nyuma na kukung’uta Toulouse 2-1 katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) ugani Parc des Princes na kufungua mwanya wa alama nane kileleni mwa jedwali.

Toulouse waliwekwa kifua mbele na Branco van den Boomen kupitia mpira wa ikabu katika dakika ya 20. Hata hivyo, PSG walisawazisha mambo kupitia kwa Achraf Hakimi kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa kipindi cha kwanza kupulizwa kisha Messi akafunga goli la ushindi kutoka hatua ya 25 katika dakika ya 58.

Ushindi huo uliwadumisha PSG kileleni mwa jedwali la Ligue 1 kwa alama 54 points kutokana na mechi 22 na sasa wanajivunia pengo la alama nane kati yao na nambari mbili Olympique Marseille.

PSG walikosa huduma za Kylian Mbappe na Neymar katika mchuano huo dhidi ya Toulouse kwa sababu ya majeraha. Toulouse sasa wanakamata nafasi ya 12 jedwalini kwa alama 29 sawa na Reims.

Bao la Messi lilikuwa lake la 10 katika Ligue 1 msimu huu na la 15 kwa jumla katika mashindano yote ya msimu huu. Marseille watapunguza pengo la alama kati yao na PSG hadi tano iwapo watazamisha chombo cha Nice mnamo Februari 5, 2023 kabla ya kuvaana na PSG katika hatua ya 16-bora ya Coupe de France wiki ijayo.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Jumamosi):

PSG 2-1 Toulouse

Troyes 1-3 Lyon

Rennes 1-3 Lille

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Newcastle United na West Ham nguvu sawa katika EPL ugani St...

Wolves wang’ata Liverpool na kuendeleza masaibu ya...

T L