• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Lucy Murigi aibuka mshindi wa mbio za kupanda mlima mita 2,394 nchini Ufaransa

Lucy Murigi aibuka mshindi wa mbio za kupanda mlima mita 2,394 nchini Ufaransa

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa zamani wa dunia Lucy Murigi aliibuka malkia wa duru ya tatu ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Mbio za Milimani Duniani (WMRA) ya Montee du Nid d’Aigle katika eneo la Saint-Gervais-Les-Bains nchini Ufaransa, Julai 17.

Katika mbio hizo zilizovutia washiriki 500 na kuanzia katika mwinuko wa mita 596 katika eneo la Parc Thermal Le Fayet na kumalizikia katika mwinuko wa mita 2,394 wa Refuge du Nid d’Aigle, Murigi alikamilisha mbio za umbali huo wa kilomita 19.3 kwa muda wa saa 2:06:08.

Mkenya huyo, ambaye alikosa rekodi ya dunia inayoshikiliwa na Mfaransa Isabelle Guillot tangu 2006 kwa sekunde mbili, alifuatiwa kwa karibu na Wafaransa Christel Dewalle (2:06:29) na Anais Sabrie (2:07:34) mtawalia.

Waitaliano Xavier Chevrier (saa 1:44:25), Francesco Puppi (1:45:49) na Henri Aymonod (1:46:44) walifagia nafasi tatu za kwanza katika kitengo cha wanaume, mtawalia. Chevrier alifuta rekodi ya 1:47:49 ambayo Manu Meyssat aliweka mwaka 2017. Duru ya nne Tatra SkyMarathon itaandaliwa nchini Poland mnamo Julai 24.

You can share this post!

JAMVI: Dalili mwafaka umepatikana Mlimani kuhusu kura ya...

CAF yaunga mkono pendekezo la Kombe la Dunia kuandaliwa...