• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 8:09 PM
Macho kwa Japan, Uhispania Kombe la Dunia la Wanawake likiingia 16-bora

Macho kwa Japan, Uhispania Kombe la Dunia la Wanawake likiingia 16-bora

NA MASHIRIKA

SYDNEY, Australia

JAPAN na Uhispania wanapigiwa upatu kunyanyasa Norway na Uswisi kwenye Kombe la Dunia la Wanawake linaloingia 16-bora mtawalia, Jumamosi.

Mabingwa wa 2011 Japan wanaojivunia kuwa na mfumaji matata Hinata Miyazawa walitamalaki Kundi C baada ya kulipua Zambia 5-0, Costa Rico 2-0 na Uhispania 4-0.

Walikuwa wamebomoa Panama 5-0 katika mechi yao ya mwisho kabla ya kombe hilo la mataifa 32.

Matokeo hayo yanatarajiwa kuwa motisha tele kwa Japan walio na rekodi nzuri dhidi ya washindi wa 1995 Norway.

Katika mechi nane zilizopita, Norway ililemea Japan 4-0 kwenye Olimpiki (Julai 1996) na 4-0 katika Kombe la Dunia (Juni 1999) na 2-0 katika Kombe la Algarve (Machi 2013).

Norway wamepoteza tano zikiwemo 2-0 katika Kombe la Algarve (Machi 2017) na 4-1 katika mechi ya kirafiki (Novemba 2018). Sophie Roman Haug aliyetetemesha nyavu za Ufilipino mara tatu katika ushindi wa 6-0 makundini, atategemea na Norway.

Wahispania walipepeta Uswisi 3-2 Oktoba 2011 na kupoteza 4-3 Juni 2012 katika Kombe la Ulaya kabla ya kutawala 2-0 katika kipute cha Algarve mwaka 2019 kwa hivyo wana rekodi nzuri.

Macho yatakuwa kwa mshambulizi wa Paris Saint-Germain Ramona Bachmann kuongoza mawindo ya Uswisi dhidi ya Uhispania inayojivunia ‘muuaji’ Jenni Hermoso. Jenni anaongoza katika kufungia Uhispania mabao mengi (50).

  • Tags

You can share this post!

LSK yapinga Sheria ya Fedha ya 2023

Wanafunzi walioendea slesi za ziada shuleni waadhibiwa...

T L