• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 6:50 AM
Mallorca yaduwaza Real Madrid katika pambano la La Liga

Mallorca yaduwaza Real Madrid katika pambano la La Liga

Na MASHIRIKA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Real Madrid, walipoteza fursa ya kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi Barcelona baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Mallorca ugani Son Moix mnamo Jumapili.

Kiungo matata wa Real, Marco Asensio, alipoteza penalti katika mechi hiyo dhidi ya Mallorca ambao ni waajiri wake wa zamani.

Vedat Muriqi aliwaweka wenyeji Mallorca uongozini baada ya kombora lake kumbabatiza beki Nacho Iglesias na kushuhudia mpira ukijaa wavuni katika dakika ya 13.

Penalti ambayo Real walipewa katika dakika ya 59 ilitokana na tukio la kipa Predrag Rajkovic kumchezea Vinicius Junior visivyo ndani ya kijisanduku. Hata hivyo, Rajkovic alipangua mkwaju huo wa Asensio na kuhakikisha kwamba waajiri wake wanaondoka ugani na alama tatu muhimu.

Huku matokeo hayo yakidumisha Real katika nafasi ya pili jedwalini kwa alama 45, Mallorca nao walisalia katika nafasi ya 10 kwa pointi 28, moja pekee nyuma ya Athletic Club Bilbao, Rayo Vallecano na Osasuna.

Ushindi wa Mallorca ulikuwa wao wa kwanza dhidi ya Real almaarufu Los Blancos tangu 2019 na wa pili dhidi ya miamba hao wa soka ya Uhispania katika mechi 14.

Mallorca almaarufu Los Piratas waliwahi pia kutandika miamba Atletico Madrid 1-0 katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa La Liga ugani Son Moix msimu huu wa 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kaunti yampa mjenzi miezi 3 kumaliza kituo cha kutibu kansa

Chepng’etich arejea mbio za nyika kwa kishindo,...

T L