• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:29 PM
Kaunti yampa mjenzi miezi 3 kumaliza kituo cha kutibu kansa

Kaunti yampa mjenzi miezi 3 kumaliza kituo cha kutibu kansa

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI ya Kaunti ya Taita Taveta, imempa mkandarasi miezi mitatu kukamilisha ujenzi wa kituo maalumu cha kutibu ugonjwa wa saratani.

Ujenzi huo ukikamilishwa itakuwa ni afueni kwa wagonjwa wanaouguza saratani ambao hulazimika kupewa rufaa hadi katika Hospitali Kuu ya Pwani iliyo Mombasa.

Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani, katika Taasisi ya Teknolojia ya Pwani (CIT), Gavana Andrew Mwadime aliwasihi wakazi waende katika vituo vya afya kupimwa iwapo wana saratani ili kuanza matibabu mapema.

“Huu ugonjwa ndio unaathiri watu wengi zaidi ndio maana tumeanza kujenga kituo malaum cha saratani. Tumempa mwanakandarasi siku 150 akamilishe haraka ili wananchi wafaidike,” akasema Bw Mwadime.

Naibu Gavana, Bi Christine Kilalo, alisema ingawa ugonjwa huo ni jinamizi kubwa, unaweza kutibiwa ukitambuliwa mapema.

“Tunahimizana hasa kina mama twendeni kupata uchunguzi kila mwaka,” akasema Bi Kilalo.

  • Tags

You can share this post!

Utata wazidi kukumba Sekondari ya Msingi

Mallorca yaduwaza Real Madrid katika pambano la La Liga

T L