• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Man-City wapoteza alama muhimu baada ya Everton kuwalazimishia sare ya 1-1 katika EPL ugani Etihad

Man-City wapoteza alama muhimu baada ya Everton kuwalazimishia sare ya 1-1 katika EPL ugani Etihad

Na MASHIRIKA

BEKI John Stones wa Manchester City amesema alama moja iliyookotwa na waajiri wake dhidi ya Everton baada ya sare ya 1-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumamosi ugani Etihad imewatikisa pakubwa.

“Ni uchungu sana kutotia kapuni alama zote muhimu katika mechi hiyo. Ilikuwa mechi tuliyokuwa na ulazima wa kushinda ili kuendeleza presha kwa Arsenal. Lakini sasa tumepata pigo katika mbio za kufukuzia viongozi,” akasema Stones.

Matokeo hayo yaliacha Man-City katika nafasi ya pili kwa alama 36, saba nyuma ya Arsenal waliofungua mwanya wa alama saba baada ya kupepeta Brighton 4-2 ugani Amex.

Erling Haaland, aliyekabiliwa visivyo na Ben Godfrey mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, aliweka Man-City kifua mbele katika dakika ya 24 baada ya kukamilisha krosi ya Riyad Mahrez ndani ya kijisanduku.

Hata hivyo, Demarai Gray alisawazishia Everton katika kipindi cha pili baada ya kumzidi maarifa beki Rodri Hernandez katika dakika ya 64. Everton sasa wanakamata nafasi ya 15 jedwalini kwa alama 16 baada ya mechi 17 za EPL.

Ushindi kwa Man-City ungewawezesha kupunguza pengo la alama kati yao na Arsenal inayonolewa na kocha Mikel Arteta aliyewahi kuwa msaidizi wa kocha Pep Guardiola ugani Etihad.

Baada ya kutandaza jumla ya mechi 16 mnamo 2021-22, Man-City walikuwa wakiselelea kileleni mwa jedwali la EPL huku pengo la alama 12 likitamalaki kati yao na Arsenal waliokuwa wakishikilia nafasi ya sita.

Msimu huu, Man-City wanapigania taji la EPL kwa mara ya tatu mfululizo japo wamepoteza alama muhimu mara tatu zaidi kuliko Arsenal. Vikosi hivyo bado havijakutana katika EPL muhula huu.

Man-City sasa hawajashinda mechi mbili mfululizo katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad ligini licha ya kupepeta washindani mara 11 mfululizo kabla ya Brentford kuwakomoa –1 mnamo Novemba 12, 2022.

MATOKEO YA EPL (Jumamosi):

Wolves 0-1 Man Utd

Bournemouth 0-2 Crystal Palace

Fulham 2-1 Southampton

Man-City 1-1 Everton

Newcastle 0-0 Leeds

Brighton 2-4 Arsenal

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wasafiri kutoka China kuzimwa

Violet Nanjala aingia 2023 akiogopwa zaidi na makipa nchini...

T L