• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Man-City watandika Arsenal 3-1 ugani Emirates na kutua kileleni mwa jedwali la EPL

Man-City watandika Arsenal 3-1 ugani Emirates na kutua kileleni mwa jedwali la EPL

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City walirejea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2022 baada ya kusajili ushindi wa 3-1 dhidi ya Arsenal ugani Emirates mnamo Jumatano usiku.

Man-City ambao ni mabingwa watetezi wa EPL walianza kipindi cha pili kwa matao ya juu na kushinikiza mabeki wa Arsenal kufanya makosa yaliyochangia fursa za mabao muhimu.

Awali, beki Takehiro Tomiyasu alishindwa kumfikishia kipa Aaron Ramsdale mpira na hivyo kumpa kiungo Kevin de Bruyne fursa ya kuwaweka Man-City kifua mbele katika dakika ya 24. Hata hivyo, Bukayo Saka alisawazisha mambo katika dakika ya 42 kupitia penalti iliyosababishwa na kipa Ederson Moraes aliyemchezea fowadi Eddie Nketiah visivyo ndani ya kijisanduku.

Mabao mawili ya Man-City katika kipindi cha pili yalifumwa wavuni na Jack Grealish pamoja na Erling Haaland ambaye sasa anajivunia magoli 26 katika EPL muhula huu.

Kichapo kutoka kwa Man-City kiliendeleza masaibu ya Arsenal waliopigwa pia na miamba hao 1-0 katika Kombe la FA kabla ya Everton kuwakomoa 1-0 ligini na Brentford kuwalazimishia sare ya 1-1 katika EPL.

Matokeo hayo yaliwafanya kupoteza alama nane kutokana na mechi tatu zilizopita za EPL na sasa wanakatama nafasi ya pili jedwalini kwa pointi 51 sawa na Man-City ambao wametandaza mechi moja zaidi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Borussia Dortmund wapepeta Chelsea 1-0 katika hatua ya...

Ajitahidi kuwakwamua wanawake kiuchumi katika mitaa ya...

T L