• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Mkenya Shoaib Vayani achaguliwa naibu rais ulengaji shabaha Afrika

Mkenya Shoaib Vayani achaguliwa naibu rais ulengaji shabaha Afrika

Na GEOFFREY ANENE

NAIBU wa Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) Shoaib Vayani amechaguliwa kuwa naibu rais wa kwanza wa Shirikisho la Ulengaji wa shabaha kwa kutumia bunduki barani Afrika (ASSF) kwa kipindi cha kutoka 2021 hadi 2025.

Uchaguzi uliandaliwa jijini Cairo, Misri mnamo Desemba 19.

Shoaib, ambaye alikuwa mwanakamati kwenye ASSF miaka 10 iliyopita, alipata kura 16 kati ya 19 za kuwa naibu wa nne wa rais kwa miaka minane.

“Miaka 15 iliyopita, ASSF ilikuwa na mataifa saba wanachama. Sasa, idadi hiyo imefika 19 na inaendelea kuongezeka. Inafurahisha sana kutumikia mchezo huu ninaoupenda kwa moyo wangu,” Shoaib alieleza.

“Nashukuru Wizara yetu ya michezo kwa kuendelea kutupiga jeki, bodi ya kupeana leseni ya bunduki za mashindano, idara za polisi, polisi wa jinai (DCI), majeshi (KDF) na klabu nyingine zinazosaidia shughuli za ulengaji wa shabaha,” alisema na pia kuongeza kuwa NOC-K na mashirikisho yamemsaidia sana katika jukumu lake kama naibu wa katibu mkuu wa NOC-K ambayo imemsaidia ASSF.

  • Tags

You can share this post!

Jumwa asukumwa awe naibu kiongozi UDA

Waliomrarua Raila sasa wamnyenyekea

T L