• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:42 PM
Montreal yanyamazisha Seattle Sounders ligi ya MLS

Montreal yanyamazisha Seattle Sounders ligi ya MLS

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal anayochezea Victor Wanyama imerukia uongozi wa Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) baada ya kuduwaza Seattle Sounders 2-1 Juni 30.

Montreal ya kocha Wilfried Nancy ilichana nyavu za Seattle kupitia mabao mawili ya Mason Toye.

Seattle ilitangulia kutetemesha nyavu za Montreal kupitia kwa Jordan Morris dakika ya tatu. Toye alisawazisha 1-1 dakika ya 18, huku timu hizo zikienda mapumzikoni bila mabao zaidi 1-1. Toye alipachika bao la ushindi dakika ya 62.

Montreal, ambayo ilibanduliwa kwenye kipute cha Canadian Championship majuzi, imekaa juu ya MLS ukanda wa Mashariki kwa alama 29 baada ya kujibwaga uwanjani mara 17. Iko mbele ya Newy York Red Bulls na Philadelphia Union kwa tofauti ya ubora wa magoli.

Red Bulls na Philadelphia zimesakata mechi 18 na 17 mtawalia. New York City (pointi 28 kutokana na mechi 16), Orlando City (alama 25 baada ya kucheza mechi 17), Cincinnati (pointi 24 baada ya kujibwaga uwanjani mara 17) na New England Revolution (alama 24 baada kutandaza michuano 17) zinafunga mduara wa timu saba za kwanza zitakazoingia awamu ya muondoano.

Los Angeles FC inaongoza MLS Magharibi kwa pointi 36 ikifuatiwa na Austin (31), Real Salt Lake (29), FC Dallas (26) na Nashville (26). Los Angeles Galaxy na Seattle zinakamilisha timu saba za kwanza kwa alama 24 na 23 mtawalia.

  • Tags

You can share this post!

Sadio Mane na Mohamed Salah watiwa katika orodha ya...

Ruto aahidi kuokoa Wakenya kiuchumi

T L