• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Sadio Mane na Mohamed Salah watiwa katika orodha ya masogora 30 wanaowania taji la Mchezaji Bora wa Mwaka barani Afrika

Sadio Mane na Mohamed Salah watiwa katika orodha ya masogora 30 wanaowania taji la Mchezaji Bora wa Mwaka barani Afrika

Na MASHIRIKA

WASHAMBULIAJI Sadio Mane na Mohamed Salah wamejumuishwa katika orodha ya masogora 30 wanaowania taji la Mchezaji Bora wa Kiume barani Afrika mnamo 2021-22.

Mane aliyeyoyomea Ujerumani mnamo Juni 2022 kuchezea Bayern Munich, anapigiwa upatu wa kupiku Salah kwenye vita vya kuwania tuzo hiyo.

Fowadi huyo wa zamani wa Liverpool aliongoza Senegal kukomoa Misri kwenye fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) mnamo Februari 2022 nchini Cameroon kabla ya kusaidia tena kikosi hicho kubwaga Misri mnamo Machi 2022 kwenye mchujo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

Nchini Uingereza, Salah na Mane waliongoza Liverpool kushinda Kombe la FA na League Cup mnamo 2021-22 ila wakazidiwa ujanja na Manchester City kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kabla ya Real Madrid kuwapiga 1-0 kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Salah anayejivunia kutwaa taji la Mchezaji Bora wa Afrika mara mbili, aliibuka Mfungaji Bora wa EPL kwa mabao 23 sawa na Son Heung-min wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Korea Kusini.

Salah ambaye ni raia wa Misri, alituzwa Mchezaji Bora wa Msimu wa 2021-22 kutoka kwa Chama cha Wanahabari wa Soka (FWA) na Chama cha Wanasoka Wataalamu (PFA).

Zaidi ya Mane na Salah, mchezaji mwingine wa haiba kubwa katika orodha hiyo ni Riyad Mahrez wa Manchester City na timu ya taifa ya Algeria. Gambia wanawakilishwa na Musa Barrow huku Comoros wakiwa na Youssouf M’Changama. Mataifa hayo yalishiriki fainali za AFCON kwa mara ya kwanza mnamo 2022.

Senegal ambao ni mabingwa wa AFCON ndio wanajivunia idadi kubwa ya masogora wanaowania tuzo hiyo, wakiwemo Mane, Edouard Mendy (Chelsea), Nampalys Mendy (Leicester City), Saliou Ciss (Nancy) na Kalidou Koulibaly (Napoli).

Wengine ni Franck Kessie wa AC Milan na timu ya taifa ya Ivory Coast, Achraf Hakimi wa Morocco na Paris Saint-Germain (PSG) na Vincent Aboubakar wa Cameroon aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza baada ya zaidi ya miaka 50 kufunga mabao manane katika fainali moja ya AFCON.

Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetoa orodha ya kategoria mbalimbali za kuwaniwa kwenye tuzo hiyo zikiwemo Chipukizi Bora wa Mwaka na Kocha Bora wa Mwaka. Washindi watatuzwa mnamo Julai 21, 2022 jijini Rabat, Morocco.

MCHEZAJI BORA WA MWAKA (WANAUME)

§ Riyad Mahrez (Algeria & Manchester City)

§ Bertrand Traore (Burkina Faso & Aston Villa)

§ Blati Toure (Burkina Faso & Pyramids)

§ Edmund Tapsoba (Burkina Faso & Bayer Leverkusen)

§ Andre-Frank Zambo Anguissa (Cameroon & Napoli)

§ Karl Toko Ekambi (Cameroon & Lyon)

§ Vincent Aboubakar (Cameroon & Al Nassr)

§ Youssouf M’Changama (Comoros & Guingamp)

§ Franck Kessie (Ivory Coast & AC Milan)

§ Sebastien Haller (Ivory Coast & Ajax)

§ Mohamed Abdelmonem (Misri & Al Ahly)

§ Mohamed Elneny (Msiri & Arsenal)

§ Mohamed Salah (Msiri & Liverpool)

§ Mohamed El Shenawy (Msiri & Al Ahly)

§ Musa Barrow (Gambia & Bologna)

§ Naby Keita (Guinea & Liverpool)

§ Aliou Dieng (Mali & Al Ahly)

§ Hamari Traore (Mali & Rennes)

§ Yves Bissouma (Mali & Tottenham Hotspur)

§ Achraf Hakimi (Morocco & Paris St-Germain)

§ Sofiane Boufal (Morocco & Angers)

§ Yahya Jabrane (Morocco & Wydad Athletic Club)

§ Yassine Bounou (Morocco & Sevilla)

§ Moses Simon (Nigeria & Nantes)

§ Edouard Mendy (Senegal & Chelsea)

§ Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)

§ Nampalys Mendy (Senegal & Leicester City)

§ Sadio Mane (Senegal & Bayern Munich)

§ Saliou Ciss (Senegal & Nancy)

§ Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)

MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA KLABU (WANAUME)

§ Riad Benayad (ES Setif)

§ Tiago Azulao (Petro Atletico)

§ Karim Konate (ASEC Mimomas)

§ Ali Maaloul (Al Ahly)

§ Aliou Dieng (Al Ahly)

§ Mohamed Shenawy (Al Ahly)

§ Mohamed Sherif (Al Ahly)

§ Percy Tau (Al Ahly)

§ Morlaye Sylla (Horoya)

§ Achraf Dari (Wydad Athletic Club)

§ Yahya Jabrane (Wydad Athletic Club)

§ Zouhair El Moutaraji (Wydad Athletic Club)

§ Mouhcine Moutouali (Raja Club Athletic)

§ Issoufou Dayo (RS Berkane)

§ Youssou El Fahli (RS Berkane)

§ Victorien Adebayor (Niger & Union Sportive Gendarmerie Nationale)

§ Peter Shalulile (Mamelodi Sundowns)

§ Bandile Shandu (Orlando Pirates)

§ Thembinkosi Lorch (Orlando Pirates)

§ Mohamed Ali Ben Romdhane (Esperance Sportive de Tunis)

CHIPUKIZI BORA WA MWAKA (WANAUME)

§ Dango Ouattara (Burkina Faso & Lorient)

§ Karim Konate (Cote d’Ivoire & ASEC/RB Salzburg)

§ Jesus Owono (Equatorial Guinea & Alaves)

§ James Gomez (Gambia & AC Horsens)

§ Kamaldeen Sulemana (Ghana & Rennes)

§ Ilaix Moriba Kourouma (Guinea & Valencia)

§ El Bilal Toure (Mali & Reims)

§ Akinkunmi Amoo (Nigeria & FC Copenhagen)

§ Pape Matar Sarr (Senegal & Metz)

§ Hannibal Mejbri (Tunisia & Manchester United)

KOCHA BORA WA MWAKA (WANAUME)

§ Kamou Malo (Burkina Faso)

§ Amir Abdou (Comoros)

§ Carlos Quieroz (Misri)

§ Pitso Mosimane (Al Ahly)

§ Tom Saintfiet (Gambia)

§ Florent Ibenge (RS Berkane)

§ Vahid Halilhodzic (Morocco)

§ Walid Regragui (Wydad Athletic Club)

§ Aliou Cisse (Senegal)

§ Mandla Ncikazi (Orlando Pirates)

TIMU BORA YA MWAKA (WANAUME)

§ Burkina Faso

§ Cameroon

§ Comoros

§ Misri

§ Equatorial Guinea

§ Gambia

§ Mali

§ Morocco

§ Senegal

§ Tunisia

KLABU BORA YA MWAKA (WANAUME)

§ ES Setif (Algeria)

§ Petro Atletico (Angola)

§ TP Mazembe (DR Congo)

§ Al Ahly (Misri)

§ Al Ahly Tripoli (Libya)

§ Al Ittihad (Libya)

§ Raja Club Athletic (Morocco)

§ RS Berkane (Morocco)

§ Wydad Athletic Club (Morocco)

§ Orlando Pirates (South Africa)

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Kauli ya Ben Pol

Montreal yanyamazisha Seattle Sounders ligi ya MLS

T L