• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:50 AM
Mourinho apigwa marufuku ya siku 10 na kutozwa faini ya Sh7.7 milioni kwa kinywa kichafu

Mourinho apigwa marufuku ya siku 10 na kutozwa faini ya Sh7.7 milioni kwa kinywa kichafu

Na MASHIRIKA

KOCHA Jose Mourinho amepigwa marufuku ya siku 10, hiyo ikiwa adhabu kwa sababu ya kauli kali alizozitoa kumhusu refa Daniele Chiffi.

Mourinho, 60, alisema Chiffi alikuwa “refa mwovu zaidi ambaye nimewahi kukutana naye maishani mwangu” baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) iliyokutanisha waajiri wake AS Roma na Monza mnamo Mei 3, 2023.

Mbali na marufuku, mkufunzi huyo raia wa Ureno pia amepigwa faini ya Sh7.7 milioni.

Shirikisho la Soka la Italia limesema Mourinho “amepigwa marufuku ya siku 10 na hatatakiwa kujihusisha na masuala yoyote ya soka kuanzia siku ya kwanza ya kampeni za msimu ujao hadi kipindi hicho cha adhabu kikamilike.”

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Manchester United alimkosoa Chiffi vikali baada ya Mehmet Zeki Celik wa Roma kufurushwa uwanjani kwa kadi nyekundu dakika sita kabla ya mechi ya Serie A dhidi ya Monza kukamilika kwa sare ya 1-1 ugani U-Power.

Mourinho mwenyewe alionyeshwa kadi ya manjano wakati wa mchuano huo baada ya kujitetea kwamba alivalia maikrofoni wakati wa pambano hilo ili kujikinga.

Msimu wa 2022-23 ulikuwa wa panda-shuka tele kwa Mourinho aliyeonyeshwa jumla ya kadi tatu nyekundu kwa makosa ya kuzozana na maafisa wa mechi, akiwemo Chiffi mnamo Septemba 2022 dhidi ya Atalanta.

Roma waliambulia nafasi ya sita kwenye msimamo wa jedwali la Serie A mnamo 2022-23 na waliambulia nafasi ya pili katika Europa League baada ya kuzidiwa maarifa na Sevilla kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali.

Msimu mpya wa 2023-24 katika Serie A utaanza rasmi wikendi ya Agosti 19-20.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Ofa ya Arsenal kusajili Declan Rice kwa Sh18.7 bilioni...

Korti yazima kesi iliyosukumwa na kampuni ya Gachagua...

T L