• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Mwendwa asifu programu ya FIFA na CAF kuwapa makocha mafunzo muhimu

Mwendwa asifu programu ya FIFA na CAF kuwapa makocha mafunzo muhimu

NA TOTO AREGE

MAFUNZO ya ukocha ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yalianza Jumatatu katika hoteli ya Movenpick jijini Nairobi.

Mafunzo hayo yanalenga kukuza ujuzi wa makocha na kuimarisha soka nchini.

Hafla hiyo iliongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini (FKF) Nick Mwendwa.

“Katika utawala wangu, tumekuwa makini sana kuhakikisha tunazidi kuwafunza makocha na tunafanya hivi kwa walimu wetu wa wakufunzi. Ili kuwa na wachezaji bora, kuna haja ya kuwa na makocha walioelimika vyema. Programu hii inaendana na jukumu la FKF la kutoa mafunzo kwa makocha kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa,” alisema Mwendwa.

“Wengi wetu tunapuuza umuhimu wa waalimu wa makocha, hivyo ikiwa tunaweza kukuza mwalimu mmoja mzuri wa makocha, basi tutakuwa tumetimiza malengo yetu.  Programu hii imeandaliwa na FIFA kwa ajili ya kuendeleza mafunzo rasmi kwa waelimishaji wa makocha,” alisema Meneja Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Ufundi ya FIFA Mohammed Basir.

Makocha 6,000 kutoka mashanini tayari wamepata mafunzo hayo.

  • Tags

You can share this post!

Mama mjamzito avuka mto hatari uliofurika akitafuta...

Usiporegesha mpango wa Kazi Mtaani, hawa vijana...

T L