• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Neymar atambisha PSG dhidi ya Montpellier ligini

Neymar atambisha PSG dhidi ya Montpellier ligini

Na MASHIRIKA

NEYMAR Jr alipachika wavuni mabao mawili katika ushindi wa 5-2 uliosajiliwa na waajiri wake Paris St-Germain (PSG) dhidi ya Montpellier katika gozi la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Jumamosi.

PSG walipoteza penalti kupitia Kylian Mbappe kabla ya kuwekwa uongozini na Falaye Sacko aliyejifunga. Neymar alipachika wavuni mabao mawili ya haraka na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya Wahbi Khazri na Enzo Tchato kurejesha Montpellier mchezoni. Magoli mengine ya PSG yalijazwa kimiani na Mbappe na Renato Sanches.

Pambano hilo lilikuwa la kwanza ligini kwa kocha Christophe Galiter kusimamia kambini mwa PSG mbele ya mashabiki wa nyumbani tangu aaminiwe kuwa mrithi wa Mauricio Pochettino mnamo Julai 2022.

PSG ambao ni mabingwa watetezi wa Ligue 1, walifungua kampeni za msimu huu ligini kwa ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya Clermont Foot mnamo Agosti 6, 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wachagua wanaume pekee bunge la kaunti

BI TAIFA AGOSTI 15, 2022

T L