• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
Nondies, Kabras na KCB waingia 8-bora katika duru ya Kabeberi 7s

Nondies, Kabras na KCB waingia 8-bora katika duru ya Kabeberi 7s

Na GEOFFREY ANENE

NONDESCRIPTS, Kenya Harlequin, Nakuru, Strathmore Leos, Kabras Sugar, Mwamba, KCB na Menengai Oilers mnamo Jumamosi walifuzu kushiriki robo-fainali kuu kwenye duru ya mwisho ya raga za kitaifa za wachezaji saba kila upande ya Kabeberi ugani RFUEA jijini Nairobi.

Washindi wa Tisap Sevens, Nondescripts, na mabingwa watetezi wa Kabeberi Sevens KCB pekee ndio walishinda michuano yao yote ya makundi Jumamosi.

Nondies ya kocha Benedict Nyambu ilishinda Kundi A baada ya kukung’uta Kenya Harlequin 12-7, Tessen Warriors 26-10 na Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta 22-10.

Wanabenki wa KCB, ambao wanawania taji la msimu kwenye ligi hiyo ya duru sita, walipepeta Chuo Kikuu cha Moi 50-0, Catholic Monks 35-7 na washindi wa ligi hii mwaka 2022 Menengai Oilers 10-7 katika Kundi D.

Mabingwa wa duru za Driftwood na Prinsloo Sevens Kabras wanafukuzia taji lao la pili la taifa baada ya kutawala msimu 2017.

Washindi wa Prinsloo na Christie Sevens KCB wanaotiwa makali na Andrew Amonde, walishinda msimu 2013, 2014 na 2019 nao Strathmore walinyakua taji mwaka 2009.

Kabras kutoka kaunti ya Kakamega wana alama 92, moja mbele ya KCB nao Strathmore ni nambari tatu kwa 82.

Mfalme wa mwaka 2023 atajulikana Septemba 10.

 

Matokeo ya mechi za makundi (Septemba 9):

Kundi A

Blak Blad 0 Tessen Warriors 26

Nondescripts 12 Kenya Harlequin 7

Blak Blad 5 Kenya Harlequin 31

Nondescripts 26 Tessen Warriors 10

Kenya Harlequin 28 Tessen Warriors 12

Nondescripts 22 Blak Blad 10

Kundi B

Kisumu 0 Impala 28

Strathmore Leos 5 Nakuru 5

Kisumu 0 Nakuru 28

Strathmore Leos 33 Impala 5

Nakuru 40 Impala 5

Strathmore Leos 28 Kisumu 0

Kundi C

Kabras Sugar 22 Daystar Falcons 7

Mwamba 17 Masinde Muliro 5

Kabras Sugar 17 Masinde Muliro 17

Mwamba 19 Daystar Falcons 12

Masinde Muliro 31 Daystar Falcons 0

Mwamba 10 Kabras Sugar 21

Kundi D

KCB 50 Moi University 0

Menengai Oilers 21 Catholic Monks 5

KCB 35 Catholic Monks 7

Menengai Oilers 38 Moi University 7

Catholic Monks 24 Moi University 5

Menengai Oilers 7 KCB 10

  • Tags

You can share this post!

Fountain Gates ya TZ yamsajili mshambulizi Topister Situma...

Idadi ya waliopoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi nchini...

T L