• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Olimpiki Maalum: Lynette Gitimu na Abigail Njuguna wavunia Kenya dhahabu

Olimpiki Maalum: Lynette Gitimu na Abigail Njuguna wavunia Kenya dhahabu

Na GEOFFREY ANENE

WANAGOFU Lynette Gitimu na Abigail Njuguna mnamo Ijumaa walishindia Kenya medali ya dhahabu kwenye Olimpiki Maalum zinazoendelea jijini Berlin, Ujerumani.

Walitwaa ushindi huo baada ya kuandikisha pointi 388 katika mashimo 18 ya kitengo cha tatu (D03).

Walizoa alama 96 katika raundi ya kwanza, 91 raundi ya pili, 107 raundi ya tatu na kumalisha kwa 94 raundi ya nne.

Wakenya hao wamefuatiwa na Henningsen/Mortensen kutoka Denmark (alama 480) na Chan/Poon kutoka Hong Kong (493).

Washindi wengine wa dhahabu kutoka Kenya tangu mashindano hayo yaanze Juni 17 ni wanariadha Irene Nzilani (1500m A), Daniel Mutiso (800m & 1500m A) na Purity Kandie (50m A) na waendeshaji baiskeli David Ng’ang’a (kilomita 15) na Mercy Mutuku (kilomita tano).

Walionyakulia Kenya medali za fedha ni Willis Otieno (Long Jump Standing B), Lyn Owendi na Linah Gashahun (badminton ya wachezaji wawili kila upande) na Ng’ang’a (uendeshaji baiskeli kilomita tano).

Kenya pia imepata shaba kupitia kwa Eflon King’ori na Jed Maina (badminton ya wachezaji wawili kila upande) na Anjela Nyambura (uendeshaji baiskeli kilomita tano).

  • Tags

You can share this post!

Wachimbaji madini waandamana kushinikiza mgodi ufunguliwe

Man-United wawasilishia Chelsea ofa ya tatu kwa ajili ya...

T L