• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Olunga abeba Al Duhail ligini Qatar katika ushindi dhidi ya Umm Salal

Olunga abeba Al Duhail ligini Qatar katika ushindi dhidi ya Umm Salal

Na GEOFFREY ANENE

MSHAMBULIZI Michael ‘Engineer’ Olunga amefufua matumaini ya kuhifadhi taji la mfungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Soka ya Qatar baada ya kuona lango mara mbili Al Duhail ikipepeta Umm Salal 3-1 Januari 11.

Olunga, ambaye alifunga mabao 24 kwenye ligi hiyo ya klabu 12 msimu ulipita wa 2021-2022 wakati Al Duhail ilimaliza ya pili, ana magoli saba.

Alifunga bao lake la sita msimu huu kupitia penalti dakika ya 87 na kuongeza la saba katika dakika ya tano ya majeruhi.

Umm Salal ilitangulia kuona lango kupitia kwa Valentino Yuel dakika ya 43 kabla ya Bassam Al Rawi kusawazishia Al Duhail 1-1 dakika ya 81.

Ushindi huo umeinua Al Duhail kutoka nafasi ya pili hadi uongozini. Vijana wa kocha Hernan Crespo wana pointi 20 kutokana na mechi tisa. Wako alama moja mbele ya Al Arabi iliyo na mechi moja mkononi.

Al Wakrah, ambayo ni timu pekee haijapoteza msimu huu, inapatikana katika nafasi ya tatu kwa pointi 15 baada ya kujibwaga uwanjani mara saba. Mabingwa watetezi Al Sadd wako katika nafasi ya nane kwa pointi 10 kutokana na michuano minane.

Raia wa Angola, Gelson Dala anaongoza vita vya kuwa mfungaji bora baada ya kucheka na nyavu mara nane. Nahodha wa Harambee Stars, Olunga ana magoli saba naye Yazan Al-Naimat wa Al Ahli Doha ameona lango mara sita.

  • Tags

You can share this post!

Kiini cha Naibu Rais kusimamia kahawa

TAHARIRI: KCSE: Mzozo wa usahihishaji usuluhishwe kwa hekima

T L