• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Osano analenga Tuzo ya Mnyakaji Bora muhula ujao

Osano analenga Tuzo ya Mnyakaji Bora muhula ujao

Na JOHN KIMWERE

MNYAKAJI wa Nairobi City Stars, Jacob Osano amesema amepania kupambana mwanzo mwisho kuwinda taji la mlinga lango bora kwenye kampeni za Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka ya Kenya (FKF-PL) muhula ujao.

Mchana nyavu huyo amedokeza hayo baada ya kumaliza wa pili kwenye kampeni za ngarambe ya muhula uliyokamilika wikendi iliyopita.

Mchezaji huyo alimaliza wa pili kwa kutofungwa mechi 13 naye Patrick Matasi alitwaa tuzo ya mnyakaji bora kwa kutofungwa mechi 18 baada ya kila mmoja kucheza mechi 25.

“Lengo langu ni kutwaa tuzo ya mlinda lango bora kwenye kampeni za msimu ujao,” alisema na kuongeza “nitatia bidii licha ya kujiwekea azma hiyo muhula uliopita lakini nikateleza dakika ya mwisho”.

Anashukuru kocha wa makipa Zachary Onyango kwa kuwaweka vizuri ndani ya msimu mzima.

Anadokeza ana imani wataendeleza mtindo wa kuonyesha soka safi kwenye kampeni za msimu ujao. Mchezaji huyo alipata muda mzuri kushiriki mechi za kipute hicho msimu uliopita baada ya Nicholas Muyoti aliyejiunga na klabu hiyo kufunika pengo lililoachwa wazi na kocha, Sanjin Alagic.

Muyoti anasema kuwa Osano ameonyesha kazi nzuri na anastahili kuitwa kuchezea Harambee Stars. Mchezaji huyo alichezea klabu hiyo kwa dakika 2340 kwenye mechi 26 kati ya 30 alizoshiriki.

  • Tags

You can share this post!

Mwamba RFC ni wafalme wa Driftwood 7s

Blackburn Rovers wapata kocha mpya

T L