• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Pigo kwa Liverpool na Senegal fowadi tegemeo Sadio Mane akipata jeraha baya

Pigo kwa Liverpool na Senegal fowadi tegemeo Sadio Mane akipata jeraha baya

Na MASHIRIKA

FOWADI wa Liverpool, Sadio Mane, anasubiri matokeo ya vipimo vya X-ray baada ya kupata jeraha baya alipokuwa akichezea Senegal kimataifa.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 aliondolewa uwanjani katika dakika ya 28 wakati wa mchuano uliowakutanisha na Togo kwenye soka ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

Mane alionekana kuumia ubavu au paja baada ya kukabiliwa visivyo na beki wa Togo. Ingawa hivyo, kocha wa Senegal, Aliou Cisse, amesema kuondolewa kwa Mane wakati wa mechi hiyo iliyokamilika kwa sare ya 1-1 ilikuwa hatua ya tahadhari.

Licha ya kuingia kushuka dimbani kwa ajili ya mechi hiyo wakiwa tayari wamefuzu kwa mchuajo ujao wa mwezi Machi ambapo wawakilishi watano wa bara la Afrika nchini Qatar watapatikana, Senegal walipanga kikosi imara kilichojumuisha pia kipa wa Chelsea Edouard Mendy, beki wa Napoli Kalidou Koulibaly na mshambuliaji wa Watford Ismaila Sarr.

Habib Diallo ndiye alisawazishia Senegal katika dakika ya 93. Senegal watakamilisha kampeni za Kundi H dhidi ya Congo mnamo Novemba 14, 2021. Liverpool ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa alama nne nyuma ya viongozi Chelsea wamepangiwa kumenyana na nambari tano Arsenal katika mchuano ujao wa EPL mnamo Novemba 20, 2021 ugani Anfield.

Mane amefungia Liverpool mabao manane kutokana na mechi 15 zilizopita katika mashindano yote kufikia sasa msimu huu. Anatarajiwa kukosa michuano ya Liverpool mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2022 wakati ambapo Senegal watakuwa wakishiriki fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zitakazoandaliwa Cameroon kuanzia Januari 6 hadi Februari 6.

Mane alirejea kutoka kwa michuano ya kimataifa ndani ya jezi za Senegal mnamo 2017 akiwa na jeraha la paja kabla ya kuvunjika kidole gumba kilishofanyiwa upasuaji mwaka mmoja baadaye.

You can share this post!

Nani anameza wanaume Pwani?

Aguero atakuwa radhi kustaafu soka mnamo Februari 2022

T L