• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Real Madrid wacharaza Bilbao na kutwaa taji la Spanish Super Cup kwa mara ya 12

Real Madrid wacharaza Bilbao na kutwaa taji la Spanish Super Cup kwa mara ya 12

Na MASHIRIKA

REAL Madrid walitwaa ubingwa wa Spanish Super Cup kwa mara ya 12 baada ya mabao kutoka kwa Luka Modric na Karim Benzema kuwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao mnamo Jumapili usiku nchini Saudi Arabia.

Modric ambaye ni raia wa Croatia alifungia Real bao la kwanza kabla ya mshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Ufaransa, Benzema kufanya mambo kuwa 2-0 ugani Riyadh King Fahd kupitia penalti iliyochangiwa na tukio la Yeray Alvarez kunawa mpira.

Real pia waliadhibiwa baadaye katika kipindi cha pili kwa Bilbao kupewa penalti baada ya Eder Militao kunawa mpira ndani ya kijisanduku. Hata hivyo, kipa Thibaut Courtois alipangua mkwaju huo uliochanjwa na Raul Garcia.

Ushindi wa Real ulinyima Bilbao fursa ya kuhifadhi ufalme wa taji la Super Cup walilolitwaa mnamo 2020-21. Real kwa sasa wanasalia na taji moja pekee ili kufikia idadi ya mataji 13 ya Super Cup yanayojivuniwa na Barcelona ambao ni watani wao wakuu katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

You can share this post!

Shujaa roho juu ikielekea Malaga 7s Uhispania

Wakufunzi Rooney na Martinez wamezewa mate na Everton ili...

T L