• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Vikosi vyaweka rekodi mpya Uingereza kwa kuchanja penalti 44 baada ya kuambulia sare mwishoni mwa muda wa kawaida

Vikosi vyaweka rekodi mpya Uingereza kwa kuchanja penalti 44 baada ya kuambulia sare mwishoni mwa muda wa kawaida

Na MASHIRIKA

VIKOSI vya ligi ndogo kutoka eneo la Midlands viliweka rekodi katika soka ya Uingereza kwa kupiga jumla ya mikwaju 44 katika mchuano wa kuwania taji la JW Hunt Cup mnamo Ijumaa ugani Shifnal.

Rekodi ya awali ya penalti nyingi zaidi kuwahi kupigwa katika mechi moja nchini Uingereza baada ya vikosi kuambulia sare mwishoni mwa muda wa kawaida ni mikwaju 34.

Rekodi hiyo iliwekwa katika mechi ya EFL Trophy iliyokutanisha chipukizi wa Chelsea U-23 na kikosi cha Oxford United mnamo 1989. Rekodi hiyo ilifikiwa mwaka mmoja baadaye wakati wa mechi ya Southern League Challenge Cup iliyokutanisha Tauton Town na Truro City.

Hata hivyo, ilivunjwa usiku wa Ijumaa na klabu ya Old Wulfrunians kutoka Wolverhampton na Lane Head iliyo na makao makuu mjini Bloxwich.

Baada ya mechi yao ya JW Hunt Cup kukamilika kwa sare ya 3-3, mshindi aliamuliwa kupitia penalti na vikosi hivyo vikafungana 19-18 kwa kupiga penalti katika kipindi cha zaidi ya nusu saa.

Kivumbi cha JW Hunt Cup kimekuwa kikiendeshwa tangu 1926 na fainali yake huwa ikichezewa katika uwanja wa nyumbani wa Wolverhampton Wanderers, Molineux.

Rekodi ya dunia ya penalti nyingi zaidi kuwahi kuchanjwa katika mechi moja ni mikwaju 48 iliyopigwa wakati wa mechi ya Namibian Cup kati ya KK Palace na Civic. Mechi hiyo ilikamilika kwa KK kupepeta Civic 17-16.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mashabiki waruhusiwa kuingia viwanja vya Kenya kwa mara ya...

Beki wa zamani wa Man-Utd, Patrice Evra, afichua aliwahi...

T L