• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 3:09 PM
Roho mkononi wanatenisi ya mezani wakingoja usaidizi kuhudhuria michuano ya Afrika

Roho mkononi wanatenisi ya mezani wakingoja usaidizi kuhudhuria michuano ya Afrika

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya tenisi ya mezani ya Kenya imeimarisha maandalizi ya mashindano ya Afrika kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mjini Lagos, Nigeria.

Lagos ilichaguliwa na Shirikisho la Tenisi ya Meza barani Afrika (ATTF) kuwa mwenyeji wa mashindano yatakayofanyika katika ukumbi wa Molade Okoya-Thomas mnamo Mei 22-28.

Timu ya Kenya inatiwa makali na mchezaji Kennedy Kojal, ambaye pia ni kocha, na aliyekuwa mchezaji nambari moja nchini, Anthony Mathenge.

Kikosi cha wachezaji wanaume kinajumuisha Jensen Owade, Peter Theuri, Kevin Mwangi, Brian Mutua, na Josiah Wandera.

Kile cha akina dada kina Bahati Rufina, Lisa Wele, Mary Kinuthia, Sejal Thakkar na Lydia Setey.

Washindi wa mashindano ya Afrika watajikatia tiketi kushiriki Kombe la Dunia.

Mathenge alieleza Taifa Leo katika ukumbi wa Nairobi Goan Institute kuwa matayarisho yamepamba moto. Timu hiyo ilinufaika na mazoezi ya kuweka mwili sawa juma hili kutoka kwa klabu ya michezo ya Trailblazers ukumbini Goan.

“Tumekuwa tukifanya mazoezi Goan kwa miezi kadhaa sasa na tunatumai kusafiri wikendi hii. Tunasubiri mwelekeo kutoka Shirikisho la Tenisi ya Meza Kenya (KTTA) ambalo limekuwa likiwasiliana na serikali. Motisha iko juu na tunasubiri kupata majibu kutoka kwa wahusika kuhusu mipango ya usafiri,” alisema Mathenge.

Timu ya Kenya haikushiriki mashindano ya kimaeneo mapema mwezi huu jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa sababu ya changamoto mbalimbali.

  • Tags

You can share this post!

Sifa hasi ya kiongozi asiye na msimamo yaandama Kalonzo

Kalonzo aonekena kujaa masumbuko

T L