• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Sifa hasi ya kiongozi asiye na msimamo yaandama Kalonzo

Sifa hasi ya kiongozi asiye na msimamo yaandama Kalonzo

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka ni mwanasiasa wa kipekee kutokana na hulka yake ya kubadili misimamo ya kisiasa kila wakati.

Mfano wa hivi punde unaoakisi mwenendo huu ni tangazo kwamba atawania urais. Hii ni licha ya kwamba mnamo Machi 12, 2022 alitangaza kwamba atamuungano mkono Raila Odinga katika azma yake ya kuingia Ikulu mwaka huu.

Alipoulizwa baada ya siku mbili kama angetaka ateuliwe kuwa mgombea mwenza wa Bw Odinga, Bw Musyoka alisema kuwa alijiunga na muungano wa Azimio bila masharti yoyote.

“Sikujiunga na Azimio kwa lengo la kufaidi kama mtu binafsi bali kwa lengo la kushirikiana na wenzangu kuleta uogozi bora nchini. Kwa hivyo, sikutoa masharti yoyote,” Bw Musyoka akasema kwenye mahojiano na runinga ya KTN, nyumbani kwake Tseikuru, Kaunti ya Kitui.

Lakini kuanzia Aprili, Bw Kalonzo alibadilisha msimamo huu na kuanzisha kampeni kali ya kushinikiza kuteuliwa mgombea mwenza wa Bw Odinga.

Muungano huo ulipoteua Kamati Maalum ya watu sababu kuwaalika maombi ya watu ambao wangependa kushindania nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa Bw Odinga, Bw Musyoka alipinga wazo hilo.

Kinaya ni kwamba mwandani wake wa karibu, Seneta Enoch Wambua wa Kitui alikuwa mmoja wa wanachama wa kamati hiyo.

Baadaye aliapa kutofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa, akisema hatua hiyo ni ya kumshushia hadhi. Lakini Mei 9 alijitokeza mbele ya kamati hiyo kuhojiwa.

  • Tags

You can share this post!

IEBC: 5,800 kuwania viti bila vyama

Roho mkononi wanatenisi ya mezani wakingoja usaidizi...

T L