• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Roho mkononi wanavoliboli wa Kenya wakipimwa corona Morocco

Roho mkononi wanavoliboli wa Kenya wakipimwa corona Morocco

Na GEOFFREY ANENE

TIMU za Kenya za voliboli ya ufukweni zinatarajia kupokea matokeo yao ya virusi vya corona wakati wowote nchini Morocco baada ya kupimwa Jumapili.

Ziliwasili katika eneo la mashindano mjini Agadir saa nane usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kupitia mjini Paris nchini Ufaransa na mjini Rabat. Zilipimwa virusi hivyo baada ya kutua mjini Rabat na kwa kutumia basi kwa saa sita hadi Agadir.

Timu hiyo ya wachezaji wanne wanaume na wanne wa kike itafahamu iwapo itawania tiketi ya Olimpiki baada ya kupokea matokeo ya covid-19.

“Tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji. Tulipimwa virusi vya corona punde tu tulipowasili na kuingia karantini katika hoteli yetu hadi tupokee matokeo. Kuna masharti makali hapa ya covid-10,” alisema kocha Sammy Mulinge mnamo Jumapili.

Kama mataifa mengine yatakayoshiriki, Kenya ina timu nne. Brackcides Agala atashirikiana na Gaudencia Makokha, Yvonne Wavinya na Phosca Kasisi, Ibrahim Oduor na James Mwaniki naye Brian Melly na Enock Mogeni.

Wanaume wa Kenya, ambao wanatiwa makali na kocha Patrick Owino, wataliman na Botswana, Gambia, Tunisia, Congo Brazzaville, Afrika Kusini, Cape Verde, Morocco, Tanzania, Ghana, Ivory Coast, Mali, Mauritius, Sudan, Sudan Kusini, Togo, Sierra Leone, Niger, Nigeria na Zimbabwe. Timu mbili za kwanza zitaingia awamu ya mwisho ya mashindano ya kufuzu kushiriki Olimpiki mjini Agadir.

Vipusa wa kocha Mulinge watapepetana na Gambia, Ivory Coast, Zambia, Ghana, Sudan, Sudan Kusini, Tunisia, SierraLeone, DR Congo, Mali, Mauritius na Nigeria.

You can share this post!

Wanaume wahimizwa kuwajibikia vilivyo majukumu yao katika...

Mshambuliaji Memphis Depay sasa ni mali ya Barcelona