• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
Shabiki wa Man United kwenye mizani baada ya kuahidi kumpa mwenzake wa Chelsea mkewe   

Shabiki wa Man United kwenye mizani baada ya kuahidi kumpa mwenzake wa Chelsea mkewe  

NA LABAAN SHABAAN

SHABIKI wa klabu ya soka ya Manchester United amegeuka kuwa gumzo la mitandao ya kijamii, kutokana na ahadi yake – bet, endapo timu anayounga mkono ingecharazwa mabao na Crystal Palace basi angetoa mke wake kwa shabiki wa Chelsea kwa muda wa siku mbili.

Kipenga cha mwisho kilipopulizwa, vijana wa Erik ten Hag walikuwa wamerambwa 1 – 0 ugani Old Trafford na dau la shabiki wa “Kiburi FC” liliungua, Manchester United iliposhindwa kukomboa hata bao la kusawazisha kufikia dakika ya 94.

Picha ya wawili hao ambao ni mashabiki wa Chelsea na Manchester United wakiwa wameshika kibao chenye maandishi ya ahadi ya Man-U, na mwanamke, ilienea mitandaoni mithili ya moto nyikani.

“Kama Manchester United itapoteza mechi ya kesho Jumamosi, Septemba 30, 2023 dhidi ya Crystal Palace nitamkabidhi mke wangu kwa huyu mtu wa Chelsea kwa muda wa siku mbili,” maandiko ya ahadi yake yanaelezea.

Katika mechi hiyo, licha ya Man United kuonyeshwa kivumbi kipindi cha kwanza ilijaribu kurejea kipindi cha pili na makeke japo haikufua dafu.

Ililimwa bao moja na Crystal Palace.

Mabingwa hao wa Kombe la Carabao waliambulia patupu, ambapo walipoteza mechi yao ya nne kati ya saba walizocheza msimu huu.

Kocha wa Palace Roy Hogson ndiye meneja wa kwanza kupiga Man United mara tano mfululizo katika uga wa ‘The theatre of dreams’ maarufu Old Trafford.

 

  • Tags

You can share this post!

Wakazi Tana River walalamikia kaunti kutafuna pesa za umma

Mtoto Jasmine Njoki azikwa mshukiwa mkuu wa mauaji...

T L