• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Simba Queens yaingiza Afrika Mashariki nusu-fainali CAF

Simba Queens yaingiza Afrika Mashariki nusu-fainali CAF

NA AREGE RUTH

MABINGWA wa taji la Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Simba Queens, wamejikatia tiketi ya nusu-fainali ya Ligi ya Mabingwa (CAF) ya wanawake nchini Morocco.

Wababe hao wa ligi ya wanawake nchini Tanzania, waliifunga Green Buffaloes ya Zambia mabao 2-0 siku ya Jumapili mjini Marrakech na kuwaondoa Buffaloes mashindanoni.

Viungo Opa Clement na Asha Djafar walifungia Simba bao kila mmoja dakika ya 64 na 79 mtawalia.

Wakenya Corazone Aquino na Topister Situma wako pamoja na kikosi hicho nchini Morocco. Mshambuliaji Jentrix Shikangwa, kipa Carolyne Rufaa na beki Ruth Ingotsi hawakusafiri na timu hiyo kutokana na kuchelewa kusajiliwa kwenye mashindano.

Wekundu hao wa Msimbazi, wanawakilisha ukanda wa Afrika Mashariki kwenye mashindano hayo. Walipokea kichapo cha 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya kundi B dhidi wenyeji AS FAR.

Kwenye mechi ya pili, waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia. Walihitaji ushindi wa moja kwa moja ili kuingia hatua ya nusu fainali.

Mabingwa hao wa Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSOFA) Determine, waliaga mashindano mapema baada ya kupoteza mechi zote.

FAR Rabat Women, wanaongoza jedwali la kundi B na alama tisa, Simba wanashikilia nafasi ya pili na alama sita. Green Buffaloes na Determine walimaliza nafasi ya pili na tatu na alama moja na sufuri mtawalia.

Wakati huo huo, nahodha wa Simba Opa Clement alichaguliwa kuwa mwanadada bora wa mechi kufuatia uongozi wake dhidi ya Determine Girls.

You can share this post!

TALANTA: Kiongozi wa nyimbo

Mrembo mwenye azma ya kuvuna sifa kama Lionel Messi

T L