• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
STAA WA SPOTI: Huyu hapa malkia wa uendeshaji baiskeli Kenya

STAA WA SPOTI: Huyu hapa malkia wa uendeshaji baiskeli Kenya

NA GEOFFREY ANENE

HUWEZI kuzungumzia uendeshaji wa baiskeli nchini Kenya bila kumtaja Nancy Akinyi Debe.

Mwanadada huyo ameweka Kenya kwenye ramani ya dunia.

Akinyi ni mwanafunzi wa zamani wa Shule ya Msingi ya Asego na shule za upili za Ogande na Magare katika kaunti ya Homa Bay na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta.

Kabla ya kuzamia kabisa uendeshaji wa baiskeli mwaka 2015, Akinyi alikuwa akicheza mpira wa magongo na pia soka kama mshambulizi.

Anasema alipoanza uendeshaji wa baiskeli, changamoto kubwa ilikuwa kupata vifaa vya mchezo huo ambavyo ni ghali.

Wakati huu, Akinyi anasema changamoto inayomkabili ni kupata mashindano ya nyika ya Kombe la Dunia ya Shirikisho la Kimataifa la Uendeshaji wa baiskeli (UCI).

“Hakuna mashindano ya mbio za nyika ya UCI katika eneo hili letu la Afrika,” anasema.

Kuhusu msimu 2022 ulivyomwendea, Akinyi anasema kwa jumla mambo hayakuwa mazuri kwake.

“Nilichukua muda mrefu kupata makali mwaka jana na nilipokuwa katika hali nzuri nilipata ajali mbaya. Niliumia sana bega kwenye mashindano ya Migration Gravel Race (MGR) katika eneo la Masai Mara mwezi Juni. Sikuweza kukamilisha mashindano hayo,” alieleza.

Akinyi aliyenyakua ubingwa wa mashindano ya Jubilee Insurance Live Free yaliyofahamika awali kama Grand Nairobi Bike Race, mjini Nairobi mwezi Novemba 2022.

Lengo lake kubwa ni kufuzu kushiriki michezo ya Olimpiki 2024 itakayofanyika mjini Paris, Ufaransa.

Baadhi ya mashindano Akinyi amefurahia katika taaluma ya uendeshaji wa baiskeli ni kupata medali ya shaba katika marathon kwenye michezo ya Afrika mjini Rabat, Morocco mwaka 2019.

Ameshiriki mashindano mengi ya kimataifa yakiwemo ya barabarani ya African Continental mwaka 2018 (Rwanda), 2019 (Ethiopia) na 2021 (Misri). Pia, alishiriki Kombe la Dunia 2018 (Ufaransa) na michezo ya Jumuiya ya Madola 2022 mjini Birmingham, Uingereza.

Akinyi, ambaye ameanzisha mradi wa kukuza talanta ya waendeshaji wa baiskeli kinadada, anashauri walio na ndoto ya kutafuta riziki kupitia mchezo huo kuwa mzuri na unaolipa vizuri.

Anaongeza, “Hata hivyo, si mchezo rahisi. Una changamoto tele, hasa bei ya vifaa ni ghali.”

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Marcus Rashford

Mtimkaji wa mbio fupi Makena ashinda kilomita 10 mbio za...

T L