• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Tergat kushughulikia nidhamu Olimpiki ya msimu wa baridi Beijing 2022

Tergat kushughulikia nidhamu Olimpiki ya msimu wa baridi Beijing 2022

Na GEOFFREY ANENE

RAIS wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) Paul Tergat ameteuliwa kuhudumu katika kitengo cha nidhamu cha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Ijumaa.

Kitengo hicho kitashughulikia madai ya ukiukaji wa sheria za Olimpiki ama uamuzi wowote ama nidhamu ama kanuni, masuala yanayogusa uvunjaji wa sheria zinazokataza wanamichezo kutumia dawa za kusisimua misuli, zilizotolewa na IOC ama shirikisho lolote ama kamati ya kitaifa ya Olimpiki wakati wa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi ya Beijing 2022 inayofanyika Februari 4-20.

Enzi zake kama mkimbiaji, Tergat alishinda Mbio za Nyika za Dunia mara tano, Nusu-Marathon za Dunia mara mbili pamoja na medali za fedha katika mbio za mita 10,000 kwenye Olimpiki na Riadha za Dunia na kutawala marathon kadhaa kubwa duniani na pia kuwa mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon. Tergat yuko Beijing kwa Olimpiki ya msimu wa baridi.

Kitengo hicho cha nidhamu kinasimamiwa na Denis Oswald.

  • Tags

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Mwimbaji Sam Mpole

Mekanika asukumwa jela miaka miwili kwa wizi wa injini za...

T L