• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 4:32 PM
Timu ya ufukweni leo itafahamu kama itashiriki Madola

Timu ya ufukweni leo itafahamu kama itashiriki Madola

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya wanawake ya Voliboli ya Ufukweni leo inatazamiwa kufahamu kama itapata tikiti ya moja kwa moja, kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Julai 29 hadi Agosti 8 katika chuo kikuu cha Birmingham, Uingereza.

Hii ni baada ya Shirikisho la Voliboli Afrika (CAVB) linalotazamiwa kutoa jedwali la mchezo huo. Tumaini la timu ya Kenya kupata tikiti hiyo kupitia mechi za kufuzu liligonga mwamba ilipomaliza ya tatu kwenye mashindano yaliyokamilika Jumatatu jijini Accra, Ghana.

‘Kulingana na tangazo la awali la CAVB huenda tukapata tikiti ya moja kwa moja kufuzu kushiriki kipute hicho,” meneja wa timu ya wanaume iliyoshiriki mechi za kufuzu nchini Ghana, Sammy Mulinge alisema na kuongeza hawana lingine bali wanasubiri uamuzi wa CAVB.

Timu za Kenya zilizoshiriki mashindano hayo nchini Ghana ziliondoka jana mchana na zilitarajiwa kutua nchini saa saba usiku wa kuamkia leo. Timu ya wasichana ikishirikisha, Naomi Too na Veronica Adhiambo iliibuka ya tatu iliponyuka Rwanda kwa seti 2-0 (23-21, 21-19).

Nao wanaume, James Mwaniki na Ibrahim Odour ilimaliza nne bora walipopigwa seti 2-0 (21-10, 21-09) na wenyeji Ghana. Kinyang’anyiro hicho kilishirikisha nchi tisa ikiwamo: Kenya, Gambia, Afrika Kusini, Zambia, Rwanda, Ushelisheli, Nigeria, Mauritius na wenyeji Ghana.

You can share this post!

Ulinzi Starlets yalenga kulipua KangemiI Starlets

Poland yapepeta Uswidi na kujikatia tiketi ya kuelekea...

T L