• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Trailblazers, KPA zafinya wapinzani wao katika Voliboli

Trailblazers, KPA zafinya wapinzani wao katika Voliboli

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya wanaume ya Trailblazers na Halmashauri ya Bandari ya Kenya (KPA) kila moja  ilitia kapuni alama muhimu kwenye mechi za voliboli ya ligi kuu ziliyochezewa uwanja wa Nyayo , Nairobi.

Trailblazers ya mkufunzi, Geoffrey Omondi ilizaba Kenya Army seti 3-0 nao wanaume wa KPA walivuna seti 3-0 dhidi ya Prisons Nairobi. Trailblazers inayoshiriki kipute hicho kwa mara ya kwanza ilionyesha mchezo safi lakini kiasi ilipata ushindani mkali.

Wachezaji hao walizoa alama za 25-23, 26-24, 25-19. ”Bila shaka ninashukuru wachezaji wangu wanazidi kujiongezea tumaini la kujikatia tiketi ya kushiriki fainali za muhula huu licha ya kupoteza mchezo mmoja dhidi ya KPA,” kocha wa Trailblazers alisema na kuongeza kuwa watajaribu kurekebisha makosa yao kwenye mechi zijazo.

Mshambuliaji wa Jeshi la Ulinzi (KDF), Nelson Bitok kushoto akipiga kombora walipocheza na Kenya Prisons kwenye mechi ya voliboli ya ligi kuu ya wanaume ugani Nyayo Stadium, Nairobi. KDF ilishinda seti 3-1…Picha/JOHN KIMWERE

Nayo KPA ya kocha, Sammy Mulinge iliendelea kupiga hatua iliposajili ushindi wa pili kwa alama za 25-21, 25-13, 25-10. Mkufunzi huyo alipongeza vijana wake kwa kazi nzuri waliofanya kwenye mechi walioshiriki na kuzoa alama tano.

”Tumepania kujituma kiume tuhakikishe tumefuzu kushiriki fainali za msimu huu,” akasema na kuongeza kuwa walikuwa wanatumia mechi hizo kujiandalia kipute cha Klabu Bingwa Afrika (CAVB) mapema mwezi ujao.

Kwenye matokeo mengine, Jeshi la Ulinzi (KDF) ilipiga Prisons Kenya seti 3-1 (25-23, 15-25, 17-25, 25-21, 15-09). Nayo Administration Police (AP Kenya) ilipoteza mechi ya tatu mfululizo ilipozimwa kwa seti 3-1 (20-25, 25-22, 25-20, 25-18) na Prisons Mombasa.

Jean Claude wa Trailblazers (kushoto) akipiga mpira walipocheza na Kenya Army kwenye mechi ya voliboli ya ligi kuu ya wanaume ugani Nyayo Stadium, Nairobi. KDF ilishinda seti 3-1…Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

Patrick ‘Jungle’ Wainaina kuwania ugavana kwa...

Ni ndoto isiyowezekana kwa Liverpool kutwaa mataji manne...

T L