• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Ulinzi Starlets kuvaana na Kispeed Queens kombe la FKF

Ulinzi Starlets kuvaana na Kispeed Queens kombe la FKF

NA TOTO AREGE

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Ulinzi Starlets wanaendelea na kutetea taji lao ugenini, watakapomenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Kispeed Queens katika Uwanja wa Moi jijini Kisumu mnamo Jumapili.

Wanajeshi walishinda toleo la kwanza mnamo Oktoba 2021 baada ya kulaza Vihiga Queens 2-0 kwenye Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo (ASK) huko Nakuru.

Wanajeshi hao walijikatia tiketi ya kufuzu kwa robo fainali kwa kuwazaba Soccer Sisters 18-0 katika uwanja wa Ruraka jijini Nairobi mnamo Aprili, 17, 2023.

Mshambulizi wa Ulinzi Fasila Adhiambo ataongoza safu ya ushambuliaji. Kwa sasa ndiye mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa amefunga mabao sita.

Mtaalamu wa mbinu wa Ulinzi Joseph Mwanzia anasema, kucheza katika hatua ya mtoano kunahitaji umakini mkubwa na bidii.

“Haijalishi tutafunga mabao mangapi lakini lazima tuwe waangalifu ili tusiruhusu mabao. Tunakabiliwa na timu ngumu, tunapaswa kufunga mabao na kudumisha uongozi. Muhimu zaidi ni ushindi,” alisema Mwanzia.

Siku ya Jumamosi, mabingwa watetezi KWPL Thika Queens watamenyana na wenzao wa ligi Nakuru City Queens katika uwanja wa Ruaraka jijini Nairobi.

Kibera Soccer Ladies (Divisheni ya kwanza) na Kahawa Queens (Ligi ya Mkoa) zitamenyana katika uwanja mmoja.

Kocha mkuu wa Kahawa Michael Mure ana uhakika kwamba watafuzu kwa nusu fainali.

“Wachezaji wamejiandaa vizuri na tunaombea ushindi Jumamosi. Nahodha wetu Lucy Mukhwana ana mabao matatu na tuna imani atafunga zaidi katika mechi hii. Tulikuwa na maandalizi ya kutosha na wachezaji wangu wako sawa,” alisema Mure.

Katika mechi nyingine, Royal Starlets (Division One) watakuwa wenyeji wa Kisumu All Starlets katika uwanja wa Ndura mjini Kitale.

Toleo la mwaka huu lilikuwa na timu 10 za Ligi Kuu ya Wanawake ya Kenya (KWPL), 16 kutoka Daraja la Kwanza na sita kutoka ligi za Kaunti.

Mashindano hayo yalipoingia hatua ya robo fainali, ni timu nne pekee za KWPL, timu tatu za Divisheni ya Kwanza na timu moja ya mkoa zilizofuzu hatua ya robo.

Ratiba ya Robo Fainali ya Kombe la FKF

Jumamosi

Kibera Soccer Ladies v Kahawa Queens (Ruaraka Grounds, Nairobi 12pm)

Royal Starlets v Kisumu All Starlets (Ndura Sports Complex, Kitale 13pm)

Thika Queens v Nakuru City Queens (Ruaraka Grounds, Nairobi 2:15 pm)

Jumapili

Kisped Queens Ulinzi Starlets (Moi, Kisumu 1pm)

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Miili 29 yafukuliwa idadi ya waliofariki...

Pasta Ezekiel Odero abadili nia

T L