• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Vigogo wa chess wang’aa mashindano ya Kenya Open

Vigogo wa chess wang’aa mashindano ya Kenya Open

NA AREGE RUTH 

VIGOGO wa mchezo wa Sataranji (kwa kimombo Chess), waliwahangaisha wapinzani katika mashindano ya Afrika Mashariki (EA) ya Kenya Open Chess ambayo yanafanyika katika kituo cha Sarit Expo jijini Nairobi.

Bingwa wa kitengo cha Grand Master Timur Gareyev aliibuka kidedea na alama 2,602 baada ya Kumbwaga Shiloh Tandeka wa Uganda ambaye alizoa alama 1,706.

Kwa upande mwingine Grand Master Eltaj Safarli alizoa alama 2601 baada ya kumzidi ujanja Mkenya Lawrence Kagambi ambaye alipata alama 1,700.

Mchezaji bora wa chess wa Afrika Mashariki Mganda Arthur Ssegwanyi, alijinyakulia alama 2,375 baada ya  mchezaji wa nyumbani Glen Kingoina kujizolea alama 1,642.

Upande wa wanawake, Mkenya Francisca Kagwira alini plea alama 1,257 kwa kumpiga kwa  Anzel Laubscher alama 1,762.

Mastaa Josefine Heinemann, Shrook Wafa, Wafa Shahenda waliwabwaga  Wakenya Wanjiru Kimani, Esther Sandra na Mercy Cherono mtawalia.

Mashindano hayo ambayo yalivutia zaidi ya wachezaji 400, mshindi wa jumla ataenda nyumbani na zawadi ya Sh5.3 milioni.

Mshindi wa kitengo cha Open upande wa wanaume, atatia kibindoni Sh1 milioni, huku washindi wa kwanza na wa pili watapata Sh750, 000, na 500,000 mtawalia.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji bora atatia mfukoni Sh 500,000, huku watakaoibuka wa pili na watatu watapata Sh350, 000 na Sh200, 000 mtawalia.

 Martin Gateri, Ben Magana, Ben Nguku, Robert Mcligeyo, Matthew Kamau, na Joseph Methu ni baadhi ya wachezaji bora watakaowakilisha Kenya katika kitengo cha Open. Sasha Mongeli ataongoza kikosi cha Kenya katika upande wa wanawake.

  • Tags

You can share this post!

KIKOLEZO: Amapiano sawa na homa kwa jinsi ilivyosambaa

Injera ashukuru Melrose 7s Scotland kumtambua kama shujaa

T L