• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Wakenya matumaini tele mashindano ya kutafuta tiketi ya Olimpiki ya voliboli ya ufukweni Morocco

Wakenya matumaini tele mashindano ya kutafuta tiketi ya Olimpiki ya voliboli ya ufukweni Morocco

Na AGNES MAKHANDIA

MAKOCHA Sammy Mulinge na Patrick Owino wanaamini kuwa timu za wanaume na wanawake za voliboli ya ufukweni za Kenya zina uwezo wa kufanya vyema.

Timu hizo zitashiriki mechi za raundi ya pili ya kutafuta tiketi za Olimpiki itakayoanza mjini Agadir, Morocco hapo Juni 21.

Wanaume wa Kenya, ambao wanatiwa makali na Owino, watamenyana na Botswana, Gambia, Tunisia, Congo Brazzaville, Afrika Kusini, Cape Verde, Morocco, Tanzania, Ghana, Ivory Coast, Mali, Mauritius, Sudan, Sudan Kusini, Togo, Sierra Leone, Niger, Nigeria na Zimbabwe.

Vipusa wa kocha Mulinge watakabiliana na Gambia, Ivory Coast, Zambia, Ghana, Sudan, Sudan Kusini, Tunisia, SierraLeone, DR Congo, Mali, Mauritius na Nigeria.

Timu za Kenya zilisafiri siku ya Ijumaa. Ile ya wanaume inajumuisha nahodha wa timu yote ya voliboli ya ufukweni ya Kenya, Ibrahim Oduor pamoja na James Mwaniki. Pia, kuna Enock Mogeni na Brian Melly.

Timu ya Kenya ya kinadada inajumuisha Gaudencia Makokha na Brackcides Agala pamoja na Yvonne Wavinya na Phoscah Kasisi.

Timu mbili za kwanza katika raundi hiyo ya pili zitaingia raundi ya tatu na mwisho itakayoandaliwa mjini humo. Mashindano hayo yatakamilika Juni 28.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

You can share this post!

Jamhuri ya Czech na Croatia waambulia sare kwenye gozi la...

Neymar sasa pua na mdomo kufikia rekodi ya Pele katika...