• Nairobi
  • Last Updated October 1st, 2023 9:40 PM
Wanagofu 110 kuwania taji la KCB East Africa Golf Tour Kisumu

Wanagofu 110 kuwania taji la KCB East Africa Golf Tour Kisumu

Na GEOFFREY ANENE

KLABU ya gofu ya Nyanza itakuwa mwenyeji wa duru ya sita ya mashindano mapya ya KCB East Africa Golf Tour jijini Kisumu wikendi ya Juni 10-11.

Mashindano hayo yaliyosubiriwa kwa hamu na ghamu yamevutia wanagofu 110.

Timu mbili bora zitajikatia tiketi kushiriki fainali kubwa baadaye mwaka huu 2023 katika uwanja wa Karen Country, Nairobi.

Benki ya KCB inayodhamini mashindano haya, imeshandaa duru tano.

Adrian Monari (VetLab), Amos Butit (Eldoret), Ondino Abubakar (Kakamega), Joseph Kagicha (Railways) na Alvin Mbugua (Limuru) walishinda duru hizo tano za kwanza, mtawalia.

Mkurugenzi wa Mauzo na Mawasiliano wa KCB, Rosalind Gichuru ameeleza Taifa Leo kuwa wanafurahia kuelekea Kisumu.

“Kupitia mafunzo yetu kwa wanawake na chipukizi, tumefikia zaidi ya washiriki 500. Ni lengo letu kufikia watu zaidi na pia washiriki mashindano haya yanapoendelea kushika kasi. Tunafurahia kufika umbali huu kwa sababu ni ithibati ya kujitolea kwetu na juhudi zetu tunazofanya katika gofu,” akasema.

Majuma mawili yaliyopita, Dkt Catherine Aura aliongoza timu yake iliyo na Ronald Omondi, Beatrice Otieno na Derek Mwaura kutawala mashimo tisa katika uwanja wa gofu wa Kakamega.

Nahodha wa klabu ya gofu ya Nyanza, Thomas Odongo, amesema wanakaribisha duru ya sita ya KCB East Africa Golf Tour katika kimojawapo cha viwanja vigumu nchini.

“Tunasubiri kuona jinsi wanagofu watakavyocheza katika uwanja huu. Tunatarajia matokeo mazuri,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Mke na mume wachimba shimo ndani ya ‘bedroom’ kuficha...

MCAs wa kiume Murang’a wamulikwa kwa kuwataka wenzao wa...

T L