• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Wanaraga wa Kenya wanaocheza ughaibuni wafika 10

Wanaraga wa Kenya wanaocheza ughaibuni wafika 10

Na GEOFFREY ANENE

MONATE Akuei ni mwanaraga wa hivi punde kutoka Kenya kupata klabu ya kigeni baada ya kunyakuliwa na Old Blue RFC mjini New York nchini Amerika.

Akuei, ambaye ana asili ya Sudan Kusini, lakini ni mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya baada ya familia yake kutorokea mwaka 1998, anaungana na ndugu Jeff Mutuku na Mark Mutuku pamoja na Rotuk Rahedi (wote Amerika), Andrew Siminyu (Afrika Kusini), ndugu Dominic Coulson na Cameron Coulson (wote Uingereza), Owen Ashley (Wales), Malcolm Onsando (Romania) na Toby Francombe (Scotland).

Klabu ya Old Blue, ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Amerika, ilitangaza mapema juma hili kusaini mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Top Fry Nakuru inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya (Kenya Cup).

“Old Blue RFC inafurahia kutangaza kusajiliwa kwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya Monate Akuei. Ana umri wa miaka 23 na amechezea timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji 15 kila upande na ile ya wachezaji saba kila upande,” ilisema taarifa hiyo ya Old Blue RFC kabla ya kumkaribisha.

Monate alipokea habari hizo kwa furaha akisema kuwa ataendelea kubadilisha maisha ya watu kupitia mafanikio yoyote anayopata katika safari yake na pia akamshukuru Mungu.

Mchezaji huyo alishiriki Kenya Cup mara ya mwisho mapema mwaka 2020 na kisha kuhamia Amerika ambako amekuwa kwa karibu mwaka mmoja.

  • Tags

You can share this post!

Olunga kuonyesha waajiri wake wa Al Duhail kuwa anaweza

Zuma atakiwa ajiamulie kifungo anachotaka apewe