• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Wanariadha waalikwa kushiriki Mbio za Nyika za Mombasa

Wanariadha waalikwa kushiriki Mbio za Nyika za Mombasa

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

CHAMA cha Riadha cha Kenya (AK), tawi dogo la Mombasa, kimewaalika wanariadha kutoka shule, vyuo na mashirika mbalimbali yaliyoko kaunti hiyo kushiriki kwenye Mbio za Nyika zitakazofanyika katika viwanja vya shule ya upili ya Shimo la Tewa siku ya Jumapili, Januari 8.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Anisa Abdalla amesema kuwa wamesambaza mialiko kwa Halmashauri ya Bandari za Kenya (KPA), Kenya Navy, National Youth Services (NYS) na kampuni kadhaa za kibinafsi kualika wanariadha wao kushiriki kwenye mbio hizo.

Anisa anasema kuwa wamepeleka pia mialiko kwa shule kadhaa za upili pamoja na vyuo vikuu mbalimbali kutaka viwatume wanariadha wao kushiriki katika mbio hizo zinazofanyika kwa ajili ya kuchagua timu ya Kaunti ya Mombasa itakayoshiriki Mbio za Nyika za eneo la Pwani.

Kulingana na Anisa, wakimbiaji watakaowakilisha timu ya Mombasa watachaguliwa kwenye mbio hizo za Jumapili ili kuwakilisha kaunti hiyo kwenye Mbio za Nyika za Pwani zitakazofanyika viwanja hivyo hivyo vya Shimo la Tewa High hapo Januari 15.

“Tunataka kuwasilisha timu ya wakimbiaji mahiri kwani tunataka wengi wao wachaguliwe kwenye kikosi cha timu ya Pwani kitakachoshiriki kwenye Mbio za Nyika za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Januari 22,” akasema kinara huyo wa AK Mombasa.

Anisa ametoa ombi kwa mashirika na makapuni ya kibinfasi yajitokeze kudhamini mbio hizo za Januari 8 kwani wanahitaji kuiandaa timu ya Mombasa itakayoshiriki kwenye mbio za eneo la Pwani.

“Tunataka baada ya mbio zetu za Mombasa, tuitayarishe timu ipate ushindi mbio za eneo la Pwani,” akasema.

Habari za kuaminika zinafahamisha kuwa timu za kaunti mbalimbali za Pwani zikiwemo za Kwale, Kilifi, Lamu, Tana River, Taita Taveta na Mombasa zinajitayarisha kuhakikisha wanariadha wao wanachaguliwa kwenye kikosi cha timu ya eneo hilo kushiriki michezo ya kitaifa.

  • Tags

You can share this post!

Mbinu za Ukulima: Teknolojia ya trei kukuza miche

VALENTINE OBARA: Watu kupotezwa: Serikali ithibitishe kuwa...

T L