• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Wanyama kuondoka Montreal mwezi Novemba

Wanyama kuondoka Montreal mwezi Novemba

NA JOHN ASHIHUNDU

ALIYEKUWA nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama ataagana na timu ya Montreal Impact ya Canada inayoshiriki katika mechi za Major League Soccer mwishoni mwa mwezi ujao Novemba.

Mkrugenzi wa Michezo kwenye klabu hiyo, Olivier Renard amefichua kwamba wamejaribu kumsihi kiungo huyo aendelee kuichezea timu hiyo, lakini imeshindikana.

Wanyama tayari alikuwa ametangaza kwamba ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika mwezi Disemba, lakini hakusema anakoelekea.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akitegemewa katika safu ya kiungo, mbali na kusaidia timu hiyo kutoka nusu-fainali ya michuano ya maondoano ya MLS Cup.

Staa huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na Celtic FC ambaye ameichezea klabu hiyo mara 89 tangu ajiunge nayo mnamo Machi 2020 aliisaidia kushinda ubingwa wa Canadian Cup.

Wanyama anatarajiwa kutaja anakoelekea, lakini Renard amesisitiza kwamba hataki kuendelea kuchezea Montreal.

Wanyama aliondoka Spurs mapema mwaka 2020 na kujiunga na Montreal mnamo, wakati wengi wakifikiria makali yake yalikuwa yamepunguka, lakini walimshuhudia akipepea na kuibuka kuwa mchezaji wa kutegemewa katika kikosi hicho kipya.

Aliondoka Spurs kwa njia ya kutatanika, lakini akiwa na matumaini makubwa ya kufufua taaluma yake ya kusakata boli kwa upeo wa juu.

Kuhama kwake kuliwashangaza wengi waliodhania kuwa wachezaji waliohamia huko ni waliostaafu baada ya miaka kuwapiga kisogo.

Lakini sogora huyo wa zamani wa Southampton alirejesha makali yake muda mfupi wakati huo akiwa na umri wa miaka 28, kiasi kuwafanya mashabiki kuanza kufikiria angesalia barani Ulaya ambako soka ina ushindani mkubwa.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Celtic aliwahi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa soka ya MSL. Kadhalika liwahi kutajwa Mchezaji Bora kwenye mechi yao dhidi ya DC United baada ya timu yake kushinda na kuingia raundi ya maondoano.

  • Tags

You can share this post!

Seneti kuanza kazi rasmi huku viongozi wa kamati...

Muhoozi apigwa marufuku kutoa maoni kuhusu masuala ya...

T L