• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Wolves wang’ata Leicester City ligini

Wolves wang’ata Leicester City ligini

Na MASHIRIKA

WOLVES waliendelea kuweka hai matumaini yao ya kushiriki soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao baada ya kucharaza Leicester City 2-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumapili ugani Molineux.

Chini ya kocha Bruno Lage, Wolves walifunga mabao yao kupitia kwa Ruben Neves na Daniel Podence huku Leicester wakifutiwa machozi na Ademola Lookman.

Ushindi huo wa Wolves ulikuwa wao wa tano kutokana na mechi sita za EPL mwaka huu wa 2022. Sasa wanakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa jedwali kwa alama 40, sita pekee nyuma ya nambari nne Manchester United. Nafuu zaidi kwa Wolves ni kwamba Man-United wametandaza mechi mbili zaidi kuliko 24 ambazo wao wamesakata.

Kichapo hicho kutoka kwa Wolves kiliendeleza masaibu ya Leicester ambao sasa wamejizolea alama mbili pekee kutokana na mechi tano zilizopita za EPL huku wakibanduliwa pia na Nottingham Forest kwenye Kombe la FA walilokuwa wakilitetea.

Wolves sasa wanajivunia rekodi ya kushinda mechi 12 kati ya 13 ambazo zimemilika kwa wao kufunga bao au mabao. Waliambulia sare katika mchuano huo mwingine.

Rekodi ya sasa ya Leicester ndiyo mbovu zaidi tangu wasakate jumla ya mechi sita mfululizo bila kushinda chini ya mkufunzi Claude Puel mwanzoni mwa 2019. Sasa wanashikilia nafasi ya 11 jedwalini kwa alama 27 sawa na Aston Villa.

Matokeo ya EPL (Jumapili):

Leeds United 2-4 Man-Utd

Wolves 2-1 Leicester City

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Masaibu ya Wapemba wa Kenya yakataa kuondoka

TALANTA YANGU: Rais mchoraji

T L