• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:50 AM
Afueni kwa Murungi 500 wa chama cha PNU wakimuunga

Afueni kwa Murungi 500 wa chama cha PNU wakimuunga

NA GITONGA MARETE

GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amepigwa jeki pakubwa katika azma yake ya kuchaguliwa tena, baada ya baadhi ya wanachama wa Party of National Unity (PNU) kumuunga mkono.

Wanachama zaidi ya 500 kutoka kote nchini, walisema watampigia debe kwa dhati Bw Murungi na kuahidi kuwashawishi wenzao wampigie kura.

PNU inaongozwa na Waziri wa Kilimo Peter Munya, ambaye ni mpinzani mkuu wa Bw Murungi.

Licha ya kuwa katika muungano mmoja wa Azimio la Umoja, waziri amekataa kumuunga mkono Gavana Murungi.

Mwandani wa karibu wa Bw Munya ambaye ni mwanachama wa Bunge la Afrika Mashariki, Bw Mpuru Aburi, anampigia debe Bi Kawira Mwangaza (mgombea huru) anayemezea mate kiti cha Bw Murungi katika uchaguzi wa Agosti 9.

Aidha, katika kinyang’aro hicho, Seneta Mithika Linturi anajivunia umaarufu wa chama cha Naibu Rais William Ruto cha United Democratic Alliance.

“Tumeamua kwa sababu ya umoja wa Azimio tutampigia kura Bw Kiraitu kwa sababu ndiye mgombea bora anayeweza kuipeleka Meru mbele,” alisema Bw David Kinoti, ambaye ni mwakilishi wa PNU Kaunti hiyo.

Mwakilishi wa Azimio katika Kaunti hiyo, Bw Mugambi Imanyara ambaye ni Katibu Mkuu wa Devolution Empowerment Party (DEP) aliwaongoza wanachama kufanya uamuzi huo.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Afrika ikumbatie ushauri wa Gaddafi kuwe na...

Mgombea aahidi kufufua Mumias

T L