• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Azimio kupigia debe Muriithi Laikipia

Azimio kupigia debe Muriithi Laikipia

NA JAMES MURIMI

VYAMA chini ya vuguvugu la Azimio la Umoja sasa vimeungana kupambana na mwaniaji atakayeteuliwa na UDA anayoiongoza Dkt William Ruto katika mbio za kusaka kiti cha ugavana wa Laikipia.

Viongozi wa Jubilee, ODM, PNU na KANU walikutana mnamo Jumatano jioni ambapo walimwiidhinisha gavana wa sasa Ndiritu Muriithi kutetea wadhifa huo kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Wajumbe waliokutana katika hoteli moja mjini Nanyuki, walimtaka Bw Muriithi awanie kiti hicho kupitia Jubilee wala si PNU jinsi alivyofanya katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Mrengo wa UDA utalazimika kufanya mchujo huku aliyekuwa Gavana Joshua Irungu na mbunge wa Laikipia Mashariki Patrick Mariru wakipambania tiketi ya chama.

Mwenyekiti wa Jubilee Laikipia Justus Maragara jana alisema chama hicho kimeamua kumpa Bw Muriithi tiketi ya moja kwa moja na itamfanyia kampeni ya nyumba hadi nyumba pamoja na vyama tanzu vya vuguvugu la Azimio hadi akitetee kiti chake.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa gavana anatwaa ushindi ndipo tunamkaribisha Jubilee,”akasema Bw Kibochi.

  • Tags

You can share this post!

Gavana akemea watumishi serikalini wanaotatiza Azimio

Wakulima wa kahawa wavuna mamilioni

T L