• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Gavana akemea watumishi serikalini wanaotatiza Azimio

Gavana akemea watumishi serikalini wanaotatiza Azimio

NA JAMES MURIMI

MWENYEKITI wa bodi ya kampeni za Azimio la Umoja, Ndiritu Muriithi ameonya maafisa wa serikali katika kaunti dhi – di ya kuhangaisha vyama vya kisiasa vilivyo ndani ya muungano huo.

Bw Muriithi ambaye pia ni gavana wa Laikipia, alisema baadhi ya watumishi wa serikali, wakiwemo mawaziri na makatibu wa wizara, wamekuwa wakiingilia shughuli za vyama vya kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini.

“Nawaeleza watumishi wa serikali wakome kuingilia siasa za Laikipia au katika eneo lolote nchini. Hamwezi kuingilia masuala ya siasa katika kaunti ilhali mnatumia muda mwingi mkiwa ofisini Nairobi,” akasema Gavana Muri – ithi. Bw Muriithi aliwataka maafisa wa

serikali kuheshimu maamuzi yanayofanywa na viongozi wa vyama katika kaunti. Gavana Muriithi alifoka siku chache baada ya Katibu wa Wizara ya Biashara Johnson Weru kukutana Ijumaa mjini Nanyuki na wanasiasa wanaomezea mate viti mbalimbali katika Kaunti ya Laikipia kwa tiketi ya Jubilee.

Mkutano huo ulilenga kuhimiza wanasiasa hao kupigia debe chama cha Jubilee mashinani.

Bw Weru alisema lengo lake lilikuwa kuhakikisha kuwa chama cha Jubilee kinashinda viti vyote katika Kaunti ya Laikipia. “Nilikutana na wawaniaji wa viti mbalimbali kupitia Jubilee na tulikubaliana kwa kauli moja kuwa tutaunga mkono kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga. Lakini chama cha Jubilee

kitasimamisha wawaniaji katika nyadhifa zote zilizosalia,” akasema Bw Weru.

Lakini Gavana Muriithi anataka vyama vilivyo katika muungano wa Azimio la Umoja kushauriana na kuwa na mwaniaji mmoja ili kuepuka kugawanya kura.

Bw Muriithi aliwataka wawaniaji wanaomezea mate viti kupitia muungano wa Azimio la Umoja kufanya mazungumzo ili wasimamishe wagombeaji walio na ushawishi wa kisiasa katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

“Tumewahi kutumia utafiti wa wataalamu kubaini wawaniaji wenye ushawishi. Ikiwa utafiti wa kisayansi utabaini kwamba umaarufu wako ni asilimia 2 na mshindani wako wa chama kingine kilicho ndani ya Azimio anaungwa mkono kwa asilimia 32, tafadhali kubali kumwachia,” akasema Bw Muriithi.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru afuta kikao cha ikulu ghafla

Azimio kupigia debe Muriithi Laikipia

T L