• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Chama cha Kingi chazidi kupondwapondwa kutoka pande zote

Chama cha Kingi chazidi kupondwapondwa kutoka pande zote

ALEX KALAMA NA MAUREEN ONGALA

CHAMA cha Pamoja African Alliance (PAA) kinazidi kukosolewa na makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii katika Kaunti ya Kilifi, kinapojiandaa kusimamisha wagombeaji katika uchaguzi ujao.

Chama hicho kinachoongozwa na Gavana wa Kilifi, Bw Amason Kingi, kilitangaza kuwa kiitamuunga mkono kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga kwa urais lakini kitakuwa na wagombeaji wa nyadhifa nyingine hasa maeneo ya Pwani na pia kitaifa.

Ijapokuwa viongozi wa ODM wamepokea vyema uamuzi wa Bw Kingi kumuunga mkono Bw Odinga, wamemtaka ajiandae kwa makabiliano makali katika ushindani wa viti hivyo vingine.

Viongozi wengine ambao wamejitokeza kupinga PAA ni wa vyama vya Kadu-Asili, United Democratic Alliance (UDA), na baadhi ya wazee wa kijamii.

Mbunge wa Malindi, Bi Aisha Jumwa, alidai kuwa chama hicho hakina ajenda yoyote itakayosaidia wakazi wa Kilifi.

Akizungumza wikendi katika wadi ya Dabaso eneobunge la Kilifi Kaskazini, aliwataka wananchi wasichague mtu yeyote anayewania kiti kupitia chama hicho uchaguzini.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa ODM, tawi la Kilifi, Bw Teddy Mwambire, alisema Bw Kingi asitumie kampeni za kumpigia debe Bw Odinga kuvumsha chama chake na wagombeaji wa PAA.

“Tunamruhusu kuunga mkono Baba (Bw Odinga) lakini si kukanganya watu kwa masuala ya PAA,” akasema katika mahojiano na Taifa Leo.

Baadhi ya wazee wa Mijikenda katika eneobunge la Magarini, Kilifi, waliwalaumu viongozi wa chama hicho kwa kuwatenga na kuapa kuwa hawataungana nacho.

Kupitia kwa kikundi cha Sauti ya Wazee wakiongozwa na Bw Simon Garama, walidai kuwa chama hicho pia hakijaweka wazi malengo yake kwa wakazi wa eneo hilo.

Kwingineko, viongozi wa Kadu-Asili walitaka wenzao wa PAA wajiandae kwa ushindani katika uchaguzi ujao. Wakiongozwa na katibu wa chama hicho tawi la Kilifi, Bw Jacob Kazungu, walipuuzilia mbali uvumi ulioenezwa kwamba wataunga mkono wagombeaji wa PAA.

katika uchaguzi wa Agosti.

Bw Kingi wikendi alieleza kuwa kuundwa kwa chama hicho ni kwa minajili ya kuandaa Pwani kuwa na mgombeaji urais ifikapo mwaka wa 2027.

Kulingana naye, chama hicho kina nafasi bora ya kutetea maslahi ya Wapwani ikiwa kitafanikiwa kushinda viti vingi vya ubunge.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge aahidi mabadiliko akilenga ugavana Mombasa

Mahakama ya juu yaombwa iruhusu mpango wa BBI wa...

T L