• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Hichilema aanza kazi kwa kishindo, atimua polisi na wanajeshi

Hichilema aanza kazi kwa kishindo, atimua polisi na wanajeshi

Na MASHIRIKA

RAIS mpya wa Zambia ametimua makamanda wa jeshi na kikosi cha polisi waliotumiwa na mtangulizi wake Edgar Chagwa Lungu, kugangamiza haki za kibinadamu.

Makamanda wapya wa jeshi la ulinzi na hewani pamoja na inspekta jenerali wa polisi na manaibu wao waliapishwa jana.Makamishna wote wa polisi wa mikoa walitimuliwa lakini nafasi zao hazijajazwa.

Rais Hichilema alisema viongozi wapya wa ofisi ‘lazima waweke masilahi ya wananchi mbele na watumikie nchi kwa bidii na kuzungatia haki za binadamu.

Alisema polisi lazima wafanye uchunguzi sahihi kabla ya kuwakamata washukiwa na kwamba ‘hakuna mtu anayepaswa kukamatwa kabla ya uchunguzi kukamilika’.

Hichilema ambaye aliapishwa kushika hatamu za uongozi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika, ameahidi kuzingatia haki za kibinadamu na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.

Wakati wa ibada Jumamosi, Hichilema kuwa hatalipiza kisasa kwa maafisa wa serikali ya Lungu ambao walimnyanyasa alipokuwa kiongozi wa upinzani.Alipokuwa kiongozi wa upinzani alikamatwa na kuzuliwa mara kadhaa.

Baada ya uchaguzi wa 2016 – ambapo aliibuka nafasi ya pili – alifungwa kwa zaidi ya siku 160 kwa madai ya makosa ya uhaini alipokataa kupisha msafara wa mtangulizi wake Lungu.

You can share this post!

Mgomo wa wahadhiri wasitishwa kupisha mashauriano ya...

Waislamu walaani MUHURI kuajiri ‘mtetezi wa...