• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Kenya Kwanza waita Azimio kwa majadiliano kuhusu uteuzi wa makamishna wa IEBC

Kenya Kwanza waita Azimio kwa majadiliano kuhusu uteuzi wa makamishna wa IEBC

NA NDUBI MOTURI

WAWAKILISHI wa Kenya Kwanza katika kamati ya mazungumzo ya maridhiano wakiongozwa na mwenyekiti wao George Murugara wamesema wameandikia wenzao wa Azimio La Umoja-One Kenya kwamba wako tayari kwa mazungumzo kuanzia Julai 4, 2023.

Wamesema ajenda kuu ya mazungumzo itaangazia uteuzi wa makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Wametishia kwamba upande wa Azimio usipojitokeza kamati ya uteuzi wa makamishna wa IEBC itaendelea na mchakato huo.

Naye mwenyekiti wa wanachama kutoka upande wa Azimio, Otiende Amollo amesema upande wa serikali umetishika baada ya wao kukutana na raia katika uwanja wa Kamukunji jijini Nairobi.

“Tulikaa meza ya majadiliano tukaweka wazi matakwa yetu lakini wao wakatuonyesha madharau,” akasema Bw Amollo.

 

  • Tags

You can share this post!

Mkongwe Roy Hodgson kuendelea kudhibiti mikoba ya Crystal...

Babu Owino: Ni aibu Gachagua kuwaambia wahitimu serikali...

T L