• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Kenya Kwanza wamtongoza Shahbal

Kenya Kwanza wamtongoza Shahbal

NA VALENTINE OBARA

NAIBU Rais Rigathi Gachagua, amemhimiza Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw Suleiman Shahbal (pichani), kujitenga na maandamano yanayoitishwa na Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

Hii ni baada ya kampuni ya Gulfcap inayohusishwa na Bw Shahbal, ambaye ni mwanachama wa ODM, kushirikiana na serikali kwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu Starehe, Nairobi.

“Huyu Shahal ni kiongozi katika Azimio lakini tunashirikiana naye kwa vile ana kitu cha kubadilisha maisha ya Wakenya. Wale wako kule wanataka kubadilisha maisha ya Wakenya waje washirikiane na serikali ya Ruto,” akasema Bw Gachagua jana Jumatatu.

  • Tags

You can share this post!

Watoto waachwa mataani elimu ikizidi kudorora Pwani

WANDERI KAMAU: Sauti za jamii ndogo zianze kusikika katika...

T L