• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Kinaya Ruto akiita mawaziri wanaomkosoa

Kinaya Ruto akiita mawaziri wanaomkosoa

NA WALTER MENYA

NAIBU RAIS WILLIAM RUTO ameita mawaziri watano na Baraza la Magavana kuhudhuria mkutano wa Baraza la Serikali la Bajeti na Uchumi (IBEC) na kuzua wasiwasi kuwa siasa ambazo amekuwa akiendeleza zitazuka kwenye mkutano huo.

Mkutano huo wa Novemba 22 unajiri wakati Dkt Ruto akishutumu baadhi ya mawaziri alioita, na iwapo watafika katika makazi yake rasmi eneo la Karen, Nairobi ambayo amekuwa akitumia kwa kampeni za urais kabla ya uchaguzi mkuu wa2022.

Mawaziri hao wamekuwa wakimlaumu Dkt Ruto kwa kuwalaumu huku wakisema wanafuata maagizo ya Rais Uhuru Kenyatta ambaye ametofautiana na naibu wake.

Kuna hisia huenda akatumia mawasilisho katika mkutano huo kujipigia debe kuhusu uchaguzi wa 2022.

Miongoni mwa mawaziri ambao amealika ni Charles Keter (ugatuzi), Ukur Yattani (Fedha), Prof George Magoha (Elimu), Peter Munya (Kilimo) na James Macharia ( Uchukuzi).

Naibu Rais amekuwa akilalama kuwa maafisa wa serikali wanampigia Raila debe badala ya kuwahudumia Wakenya

Vyama vya kisiasa vyatakiwa kufanya NDC kufikia Februari 2022 ili viwe na muda wa kutosha kuandaa teuzi za watakaowania nyadhifa.

You can share this post!

Meza wembe, Kibicho amwambia Ruto

Kalonzo kimya ngome yake ikivamiwa

T L