• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 4:39 PM
KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kisumu

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kisumu

NA VICTOR RABALLA

KISUMU ni jiji la tatu kwa ukubwa nchini baada ya Nairobi na Mombasa.

Ingawa mgombea wa urais wa chama cha Azimio la Umoja-One Kenya Coalition, Bw Raila Odinga anatoka katika kaunti jirani ya Siaya, Kisumu inafahamika kama ngome yake sugu.

Wagombeaji wengi wanaowania viti mbalimbali wanapenda kuegemea kwa Bw Odinga, ili kuweza kuwashawishi wafuasi wake.

Wakazi wa Kisumu hutetegemea ukulima kama vile miwa, mchele na pamba.

Wengi wao ni watu wa kujitegemea.

Gavana wa sasa Prof Peter Nyang’ Nyong’o anawania kwa awamu ya pili, sawa na mpinzani wake mkuu Jack Ranguma aliyemtangulia (2013-2017).

Baadhi ya watu mashuhuri kutoka Kaunti ya Kisumu ni mwimbaji matata Esther Akoth maarufu kama Akothee, mchekeshaji nguli Eric Omondi na mwigizaji Lupita Nyong’o ambaye ni binti wa gavana huyo wa sasa. Lupita ni mshindi wa mataji kadhaa ya kimataifa kutokana na uigizaji wake.

Aidha, Kisumu ni nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya nchi za Kigeni, Dkt Robert Ouko.

UGAVANA

Prof Anyang Nyong’o

Alizaliwa mnamo Oktoba 10, 1945.

Alishika usukani mwaka wa 2017 baada ya kumshinda Jack Ranguma ambaye alihudumu kwa miaka mitano.

Alizaliwa Ratta, katika eneo-bunge la Seme.

Ana shahada ya kwanza na ya uzamili katika masuala ya kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na Chicago nchini Marekani mtawalia.

Alikuwa mbunge wa Kisumu Rural kwa miaka 20 kabla ya kuwa seneta wa Kisumu wa kwanza mnamo 2013.

Jack Ranguma – MDG

Alikuwa gavana wa kwanza wa Kisumu mnamo 2013 hadi 2017.

Ana shahada ya uzamili katika Uhasibu wa kimataifa na mifumo ya usimamizi na teknolojia.

Kabla ya kuingia siasani, Bw Ranguma alifanya kazi kama mhasibu kwa takriban miaka 30.

Beryl Mesoh – HURU

Ni mfanyabiashara. Hakuna maelezo kumhusu. Taifa Leo iligundua jina lake katika nyaraka za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), lakini hakuna hata karatasi moja ya kampeni katika kaunti nzima.

MAENEOBUNGE

KISUMU CENTRAL

Fred Ouda (HURU)

Joshua Oron (ODM)

Zablon Awange (HURU)

Victor Radido (HURU)

KISUMU EAST

Shakeel Shabir (HURU)

Nicholas Oricho (ODM)

KISUMU WEST

Olago Aluoch (MDG)

Rozah Buyu (ODM)

NYAKACH

Aduma Owuor (ODM)

Polyns Ochieng Daima (HURU)

Vincent Kodera (HURU)

Justus Aloo (HURU)

Stephen Ogalo (HURU)

Christopher Ondiek (DAP-K)

Okoth Opande (HURU)

Julius Omondi (UDP)

NYANDO

Jared Okello (ODM)

Charles Opiyo

Patrick Ouya

Patrick Lumumba (UDA)

Willis Orowe (MDG)

Mary Otieno (Jubilee)

MUHORONI

Onyango K’Oyoo (ODM)

Francis Ong’elle (Jubilee)

Seth Okello (UDA)

Collins Omondi (HURU)

SEME

James Nyikal (ODM)

Kadiri Hagai (HURU)

Julius Owino (HURU)

USENETA

PROF TOM OJIENDA – ODM

Alikuwa rais wa chama cha wanasheria nchini na mwakilishi wao katika tume ya huduma za mahakama.

DKT ENOCK OKOLO – JUBILEE

Ni mwanasayansi wa utafiti na mhadhiri katika Great Lakes University of Kisumu.

WAWANIAJI WA KITI CHA MWAKILISHI WA KIKE

RUTH ODINGA – ODM

Ni kitindamimba wa mzee Jaramogi Oginga Odinga.

Akiwa anatoka familia ya wanasiasa, ni dadaye mwaniaji urais wa Azimio la Umoja na ODM, Raila Odinga, na Dkt Oburu Oginga.

Alikuwa naibu wa gavana wa Kisumu mnamo 2013 hadi 2017.

Anasema kwanza anawania ili kaka yake asisemekane huwa anampa ajira. Pili, anaamini atavutia wawekezaji na kuwasaidia wanawake na vijana wa Kisumu wainuke kiuchumi.

DKT ROSE KISIA  – HURU

Alikuwa Waziri wa Utalii katika Kaunti ya Kisumu.

Mwaka 2017 alitaka kuwania useneta lakini akashindwa katika mchujo wa ODM, na Fred Outa aliyeshinda wadhifa huo baadaye.

Hapo awali alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga.

Anasema lengo lake kuu ni kuhakikisha kaunti hii inajisimamia kiuchumi, na kuunda nafasi za ajira kwa maelfu ya vijana.

VALENTINE ANYANGO OTIENO

Ana umri wa miaka 22.

Alisomea ualimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Kabla ya kujitosa katika siasa, alikuwa mwalimu katika Shule ya Upili ya Kisumu Boys.

Katika kampeni zake ana manifesto yenye hoja 14 zinazojumuisha; vituo vya kulea watoto bila malipo, vituo vya watu kuchangia na kupata maarifa ya biashara, mpango wa kukuza vipaji vya wasanii, na mpango wa kuwapa mikopo akina mama wanaofanya biashara ndogo.

PHILGONA AYUGI – UDA

Tangu aidhinishwe na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), amekuwa akikutana na vikundi mbalimbali vya wanawake Kisumu.

Ingawa hajaonekana akifanya kampeni kwenye mikutano ya kisiasa, amekuwa akizunguka katika maeneo ya Awasi, Nyahera, Kibos na kwingineko akizungumza na wakazi ana kwa ana.

Ajenda yake ni kuinua mapato ya wakazi wa kaunti hii, kutetea masomo ya wasichana na kuwaletea maendeleo.

  • Tags

You can share this post!

PAA sasa yamezwa na Kenya Kwanza, yashindwa kupaa

Mivutano yatishia kampeni za Ruto

T L