• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 1:09 PM
Malala akubali kushindwa akipongeza IEBC kwa kazi nzuri

Malala akubali kushindwa akipongeza IEBC kwa kazi nzuri

NA CHARLES WASONGA

MGOMBEA ugavana wa Kakamega kwa tiketi ya chama cha Amani National Congress (ANC) Cleophas Malala amekubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika Agosti 29, 2022.

Bw Malala, aliyewania kiti hicho chini ya mwavuli wa muungano wa Kenya Kwanza (KKA), alibwagwa na mgombeaji wa ODM Fernandes Barasa aliyezoa jumla ya kura 192,929.

Naye Malala, ambaye ni seneta anayeondoka wa Kakamega, alipata kura 159,508.

Akiongea baada ya Bw Barasa kutangazwa mshindi mnamo Jumanne Agosti 30, Bw Malala pia aliipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kazi nzuri akisema uchaguzi huo uliendeshwa kwa njia huru na haki.

“Tumekubali kushindwa, vichwa vyetu vikiwa juu. Nawapongeza wapinzani wangu Ferdinand Barasa na Ayub Savula. Hakuna kura iliibwa katika kaunti ya Kakamega. Napongeza IEBC kwa kazi nzuri,” akasema.

Uchaguzi huo ambao uliahirishwa kutoka Agosti 9 kutokana na hitilafu kwenye karatasi za kupigia kura, ulishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza kushiriki.

Bw Malala alisema kuwa yu tayari kuwasilisha sehemu yoyote ya manifesto yake kwa Gavana Mteule Barasa ili atumie kuendeleza utekelezaji wa ajenda yake ya kuboresha kaunti ya Kakamega.

Alielezea kujitolea kwake kufanya kazi na gavana huyo mpya wa Kakamega huku akiwapongeza wakazi waliojitokeza kumpigia kura.

  • Tags

You can share this post!

Ujumbe wa UN kukagua kituo cha nyuklia Ukraine

Sarai na Malala washindwa kuhimili mawimbi ya Azimio 001 na...

T L